Marekani-NBA

Mchezaji wa Kikapu-NBA Marekani ajitangaza shoga, Rais Obama ampongeza

RFI

Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani mwenye asili ya Afrika Jason Collins amejitangaza kuwa yeye ni shoga hatua ambayo imewashitua watu wengi hususani wapenzi wa mchezo huo.

Matangazo ya kibiashara

Jason Collins anakua mchezaji wa kwanza wa kimataifa mwanaume ambaye bado anacheza mpira wa kikapu kutangaza kuwa ni shoga huku akisema kuwa yeye ni mwanamme mweusi na ni shoga.
 

Rais wa Marekani Barack Obama amempongeza mwanababa huyo shoga mwenye umri wa miaka 34 anayecheza katika ligi ya NBA kwa kujitangaza hadharani.
 

Rais Obama ambaye mwaka jana alitangaza kuunga mkono ndoa za mashoga alimpigia simu Collins na kumpongeza kwa ujasiri alioonyesha na amesema atamuunga mkono.
 

Mchezaji wa zamani wa NBA John Amaechi mwaka 2007 alijitokeza hadharani na kutangaza kuwa ni shoga lakini yeye alifanya hivyo akiwa tayari amestaafu kucheza kikapu.
 

Naye Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alimpigia simu Collins na kusema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa wanamichezo wa kimataifa na ni historia kwa jumuiya ya mashoga na wasagaji.
 

Binti wa Bill Clinton, Chelseea ambaye amesema kuwa alimfahamu Collins wakati wakiwa wanachuo katika chu kikuu cha Stanford na meandika katika ukurasa wake wa tweeter kwamba anaona fahari kubwa kwa rafiki yake Collins kwa kuwa na ujasiri wa kuwa mchezaji pekee wa NBA shoga na kuweka hadharani hali yake.