Marekani

Rais Obama asema serikali yake haitavumilia kashfa za ubadhirifu

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama politico.com

Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali yake haiwezi kuvumilia kashfa inayowakabili wanafanyakazi wa kitengo cha kukusanya kodi wanaodaiwa kuwa wabadhirifu. 

Matangazo ya kibiashara

Obama ametoa tamko hilo baada ya uchunguzi uliofanyika nchini humo kuwataja waziwazi wafanyakazi hao wamekuwa wakihusika kwenye ubadhirifu na kuchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kupatikana kwa mapato sahihi.

Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Eric Holder akajitokeza mbele ya Wanahabari na kulazimika kutolea ufafanuzi kile kinachofanyika baada ya kutajwa uwepo wa ubadhirifu unaofanywa na wafanyakazi wa kitengo cha kodi.

Aidha rais Obama ameagiza kushikiliwa kwa wale wote wanaohusika na tuhuma hizo za ubadhirifu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.