Marekani-MAUAJI

Uchunguzi unaendelea kujuwa sababu za mashambulizi ya watu 13 jijini Washington na mwanajeshi wa zamani wa Marekani

eneo la tukio la mauaji na picha ndogo ni muhusika wa mauaji hayo Aaron Alexis
eneo la tukio la mauaji na picha ndogo ni muhusika wa mauaji hayo Aaron Alexis freep.com

Mamlaka zinazo endesha uchunguzi kuhusu tukio la shambulio kwenye ofisi za jeshi la wanamaji jijini Washington ambapo watu 13 walipoteza maisha huku wengine wanane wakijeruhiwa, wamefahamisha kwamba mshambuliaji alikuwa ni mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Mea wa jiji la Washington Vincent Gray amesema hakuna ushahidi ambao unaonyesha kwamba kulikuwa na mshambuliaji zaidi ya mmoja, licha ya kwamba hilo pia linawekana.
Upande wake mkuu wa polisi jijini hapo Cathy Lanier amesema wana uhakika kwamba mshambuliaji ambaye amesababisha vifo vya watu, alikuwa ni mmoja.

Mshambuliaji ambaye alipigwa risase na walinda usalama alijulikana kwa jina la Aaron Alexis, Mmarekani mweusi anakadiriwa kuw ana umri wa miaka 34 raia wa mji wa Fort Worth mjini Texas ambaye alikuwa katika jeshi la wanamaji katika mwaka wa 2007 hadi 2011.

Shambulio hilo lililotokea mjini kati, ni kubwa kuwahi kutokea katika majengo ya jeshi tangu mwaka 2009 katika kituo cha Fort Hood mjini Texas ambapo watu 13 walipoteza maisha.
Shirika la Hewlett-Packard ambako alikuwa anahudumu muhusika huyo wa mauaji, imesema kwamba Aaron Alexis alikuwa mfanyakazi katika shirika hilo kwenye kitengo cha kompyuta ambaye alikuwa anahusika na jukumu la kuweka hewani mtandao wa US Navy na Marines.

Polisi nchini Marekani imetowa tangazo kwa umma ya kutafuta taarifa zozote kuhusu shughuli za muuaji huyo, kuhusu mawasiliano yake, watu wa karibu naye na aliyoyafanya kabla ya kutekeleza mauaji hayo.

Hadi sasa haijulikani sababu zilizomfanya mwanajeshi huyo wa zamani wa Marekani kutekeleza mauaji hayo