AFGHANISTAN-Uchaguzi

Malumbano yajitokeza kati ya wagombea urais kuhusu masuala nyeti yanayoikabili Afghanistan

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai, m'moja kati ya wagombea urais walioshiriki mjadala
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai, m'moja kati ya wagombea urais walioshiriki mjadala RFI

Wagombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza wamelumbana kwenye mjadala uliorushwa moja kwa moja kwa njia ya Televisheni, ambapo wengi wa wagombea hao wameunga mkono utiwaji saini wa mktaba wa kiusalama kati ya nchi hiyo na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Suala ka rais Karzai Kutotia saini mkataba wa kiusalama kati ya nchi yake na Marekani, ndio ilikuwa ajenda kubwa ya mjadala huo wa Televisheni ambapo mgombea Abdullah Abdullah ambaye kwenye uchaguzi uliopita alishika nafasi ya pili, akikosoa vikali hatua ya rais Karzai kutotia saini mkataba huo.

Licha ya kufanyika kwa mdahalo huo, kumekuwa na hofu ya kiusalama kuhusu kufanyika kwa amani kwa uchaguzi huo kufuatia kuuawa kwa wafadhili wawili wa juu wa kampeni za Abdullah.

“Mkataba huo wa ushirikiano na Marekani, umo katika ajenda yangu ya kuusiani iwapo ntashinda uchaguzi”, amesema Zalmaï Rassoul, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Afghanistan, akibaini kwamba mkataba huo, iwapo utazingatiwa vilivyo utadumisha usalama nchini Afghanistan.

“Tunahitaji vikosi kutoka mataifa ya kigeni vitakavyo saidia jeshi letu kudumisha usalama, baada ya kuondoka kwa vikosi vya Jumuiya ya Kujihami Nato”, amesema Qayum Karzaï, kaka wa rais wa Afghanistan Hamid Karzaï, akiomba kutia saini kwenye mkataba huo wa ushirikiano na Marekani.

Katika mjadala huo kumezungumziwa pia mchakato wa amani nchini Afghanistan, ambao wakati huu umedororo, na hatma ya waasi wa taliban. Baadhi ya wagombea wameunga mkono waasi wa taliban kushirikishwa katika ujenzi wa taifa, na wengine wamepinga.