ISRAELI-PALESTINE-Mazungumzo

Israel yatishia kuichukulia vikwazo Palestina

Kiongozi wa serikali ya Israeli Benyamin Netanyahu (wapili kulia), akizunguukwa na mawaziri wake cabinet.
Kiongozi wa serikali ya Israeli Benyamin Netanyahu (wapili kulia), akizunguukwa na mawaziri wake cabinet. REUTERS/Uriel Sinai/Pool

Viongozi wa Israeli wanakutana leo kujadili vikwazo watakavyoichukulia Palestina, baada ya PLO kundi la Mahmoud Abbas kutiliana saini ya makubaliano ya maridhiano na kundi hasimu la Hamas ja na jumatano, redio ya serikali imethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao hiki maalum, kunatazamiwa aina ya vikwazo ambavyo vitachukuliwa,imeendelea kutangaza redio hio ya serikali ya Israeli, kuna uwezekano pia wa kusitisha mazungumzo moja kwa moja na viongozi wa Mamlaka ya wapalestine, mazungumzo ambayo yanasimamiwa na Marekani tangu yalipoanza julai mwaka jana, licha yakua bado yanadorora.

Mkuu wa ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu amekithibitishia kituo cha habari cha Ufaransa AFP kwamba kikao hicho cha baraza la kitaifa la usalama kitafanyika kwa usalama wa Israeli na wananchi wake.

Mkuu huyo ameyaita makubaliano hayo kati ya PLO na Hamas kwamba ni ukiukwaji mkubwa wa mazungumzo kati ya Israeli na Palestina, akibaini kwamba uongozi wa Mamlaka ya wapalestina unaIingiza Palestina katika hatari, baada ya kusaini makubaliano ya maridhiano na Hamas, huku akijizuia kutoa taarifa zaidi kuhusu vikwazo vitakavyochukuliwa dhidi ya Palestina katika kikao hicho.

Israeli imeguswa sana tangu jana na makubaliano hayo kati ya makundi hayo mawili hasimu, na kufuta kikao cha kujadili uwezekano wa kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Palestina, ambacho kilikua kimepangwa kufanyika jana jioni.

Rais wa malaka ya wapalestina, Mahmoud Abbas.
Rais wa malaka ya wapalestina, Mahmoud Abbas. REUTERS/ Mohamad Torokman

Kiongozi wa Mamlaka ya wapalestina, Mahmoud Abbas, amesema kwamba makubaliano kati ya PLO na Hamas sio kikwazo kwa mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestini, huku akithibitisha kwamba Palestina imejikubalisha kushiriki mchakato wa amani kulingana na taratibu za kimataifa.

Marekani ambayo inalichukulia kundi la Hamas kama kundi la kigaidi, imebaini kwamba makubaliano hayo kati ya makundi hayo mawili “yanaweza kabisa kutatiza” jitihada za mchakato wa amani.

PLO, ambayo inajulikana kimataifa kama ndio inawakilisha raia wa Palestina na Hamas ambayo inatawala katika ukanda wa Gaza, wameafikiana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa mnamo majuma matano yajayo.