Mahabusu wawashikilia mateka watu 122 waliokwenda kuwatembelea ndugu zao gerezani
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mahabusu katika gereza kaskazini Mashariki mwa jimbo la Sergipe nchini Brazil wameshikilia mateka 122 jana Jumamosi karibu wote walikwenda kuwatembelea ndugu zao ambao ni mahabusu ,afisa magereza ameiambia AFP.
Msemaji wa gereza Sandra Melo amesema kuwa ghasia hizo zimetokea katika upande moja wa gereza, na kuongeza kuwa kwa sasa hali imetulia na kwamba mazungumzo kwa ajili ya kuachiwa kwa mateka hao yataanza tena mapema leo Jumapili.
Melo alisema kuwa kulikuwa na walinzi wanne wa gereza miongoni mwa mateka hao katika gereza la Advogado Jacinto Filho katika mji wa Aracaju, mji mkuu wa jimbo la Sergipe.