AFGHANISTAN-MAREKANI-Usalama

Afghanistan: Gari la ubalozi mdogo wa Marekani lashambuliwa

Askari wa Afghanistan wakijaribu kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye shambulio la nje ya ubalozi wa Marekani mjini Herat, Septemba 13 mwaka 2013.
Askari wa Afghanistan wakijaribu kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye shambulio la nje ya ubalozi wa Marekani mjini Herat, Septemba 13 mwaka 2013. Reuters

Watu wawili wamejeruhiwa mapema leo asubuhi katika shambulio dhidi ya gari ya ubalozi mdogo wa Marekani katika jimbo la Herat katika mji muhimu wa mashariki mwa Afghanistan kushambuliwa na watu wasiyojulikana.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linatekelezwa siku tano baada ya shambulio lingine dhidi ya ubalozi mdogo wa India katika mji huo wa Herat, na siku moja kabla ya pendekezo la rais wa Marekani, Baracka Obama la kubakiza baadhi ya wanajeshi nchini Aghanistan hadi mwaka 2016.

Gari hlo la ubalozi mdogo wa Marekani lilikua likijielekeza katika uwanja wa ndege wa Herat, na baadae kushambuliwa na watu wasiyojulikana ambao walikua kwenye pikipiki, viongozi tawala katika mji wa Herat wamethibitisha.

Afisa mmoja wa ubalozi mdogo wa Marekani katik mji wa Herat, ambae hakutaka jina lake litajwe, amesema kwamba maafisa wawili wa usalama kwenye ubalozi huo, ambao ni wageni wamejeruhiwa katika shambulio hilo, bila hata hivo kubaini iwapo ni raia wa Marekani.

Eneo la mafunzo ya kijeshi la kundi la al Qaida, nchini Afghanistan, mwaka 2007. Picha hii ilinaswa na satelaiti.
Eneo la mafunzo ya kijeshi la kundi la al Qaida, nchini Afghanistan, mwaka 2007. Picha hii ilinaswa na satelaiti. Reuters

Hivi karibuni rais wa Afghanistan Hamid Karzai alifahamisha kwambaalipata taarifa zinazoeleza kwamba shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa India, lilitekelezwa na kundi la wanamgambo wa kislamu la Lashkar-e-Taiba (LeT) linaloendesha harakati zake nchini Pakistan, lakini mmoja wa viongozi wa kundi hilo alikanusha tuhuma hizo dhidi yao.

Barack Obama, katika kambi ya wanajeshi wa Marekani mjini Bagram, nchini Afghanistan.
Barack Obama, katika kambi ya wanajeshi wa Marekani mjini Bagram, nchini Afghanistan. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais Barrack Obama amesema kufikia mwisho wa mwaka huu, ni wanajeshi 9,800 ndio watakaosalia nchini Afganistan kuendelea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afganistan na kusaidia kupambana na visa vya ugaidi.

Obama amesisistiza kuwa maelfu ya wanajeshi wa Marekani ambao wamekuwa nchini Afghanistan watarudi nyumbani kufikia mwisho wa mwaka huu, na wale watakaosalia wataendelea kuisaidia Afgnaistan hadi mwaka 2016.

Marekani ilituma maelfu ya wnajeshi wake nchini Afganaiustan mwaka 2001 kupambana na L Qeada baad aya kundi hilo kuishmabulia Marekani.