Afghanistan-Uchaguzi

Ulinzi waimarika katika mkesha wa duru ya pili ya uchaguzi nchini Afghanistani

Ashraf Ghani Ahmadzai, lMgombea kiti cha Urais katika duru ya pili  nchini Afghanistan Juni 41 répondu aux journalistes lors d’une conférence de presse le 27 avril dernier à Kaboul.
Ashraf Ghani Ahmadzai, lMgombea kiti cha Urais katika duru ya pili nchini Afghanistan Juni 41 répondu aux journalistes lors d’une conférence de presse le 27 avril dernier à Kaboul. Reuters/Omar Sobhani

Vikosi vya Polisi na jeshi nchini Afghanistan vimeimarisha usalama karika mkesha wa duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa rais na kufanya uchunguzi kwa magari yote yanayoingia na kutoka katika mji wa Kaboul na miji mingine kwa ajili ya uchunguzi wa uwezekanao wa shambulio lolote la kundi la talibani.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la Taliban lilitishia kushambulia vituo vya kupigia kura hapo kesho Jumamosi wakati wananchi watakuwa wakipiga kura kumchaguwa kati ya wagombe wawili wanaowania nafasi hiyo. Abdoullah Abdoullah msemaji wa zamani wa kamanda Ahmad shah Massoud, aduwi mkubwa wa kundi la Taliban, atapambana na Ashraf Ghani mchumi wa zamani wa benki ya dunia ambaye alipata asilimia 45 ya kura dhidi ya asilimia 31.6 ya mpinzani wake.

Abdoullah Abdoullah mgombea kiti cha urais katika duru ya pili nchini Afghanistan
Abdoullah Abdoullah mgombea kiti cha urais katika duru ya pili nchini Afghanistan REUTERS/Mohammad Ismail

Uchaguzi huo unajiri wakati huu vikosi vya wanajeshi wa majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi Nato vinavyoongozwa na Marekani vikijiandaa kuondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, baada ya kuwa nchini humo kwa kipindi cha miaka 12 ya mzozo.

Katika awamu ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika April 5 mwaka huu, kundi la Taliban haliku faulu licha ya mshambulizi ya hapa na pale kuzuia wananchi wasishiriki kwa winhi katika uchaguzi huo uliopongezwa na jumuiya ya kimataifa.

Kiongozi wa vikosi vya Usalama nchini humo Jenerali Sher Mohammed Karimi amesema wanaimani kwamba uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa licha ya uwepo wa vitisho vya aduwi ambaye amepanga kuvuruga, lakini kutokana na hatuwa walizo zichukuwa wanaimani bila shaka aduwi atashindwa kama alivyo shindwa katika duru ya kwanza.

Rais anaye maliza muda wake Hamid Karzai amevitolea wito vikosi vya usalama kutoegemea upande wowote katika uchaguzi huu, huku viongozi wa tume ya uchaguzi wakitakiwa kupiga vita uwepo wa udanganyifu wa kura kama ilviyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2009

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya ulinzi nchini humo jenerali Mohamed Zahir Azimi, takriban wanajeshi laki nne na polisi pamoja na wajumbe wa taasisi zote za usalama wamehamsishwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika katika hali tulivu.

Abdallah Abdallah juma lililopita aliponea chupuchupu katika shambulio lililolenga msafara wake, shambulio lilogharimu maisha ya watu 12 katika mji mkuu Kaboul.

Katika taarifs iliotolewa Juni 2 mwaka huu na kundi la Taliba waliwataka wannchi wote ambao hawataki kuuawa au kujeruhiwa kutosogelea vituo vya kupigia kura Juni 14 mwaka huu wakati wa duru ya pili ya Uchaguzi.