AFGHANISTA-MAREKANI-Uchaguzi-Siasa-Usalama

Afghanistan : Marekani yatishia kusitisha msaada

Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais wa Marekani, Barack Obama. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Barack Obama amewaonya wagombea wawili wa uchaguzi wa rais nchini Afghanistan Abdullah Abdullah na Ashraf Ghani kuwa machafuko au hatuwa zozote zitazo chukuliwa kinyume na katiba ya nchi hiyo zitapelekea Marekani kusitisha msaada wake kwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mawasiliano kwa njia ya sim rais Obama amewaambia viongozi hao kwamba anamatumaini ya kuona muafaka unapatikana baada ya uchunguzi wa kina kuhusu uwepo wa taarifa za udanganyifu wa kura na kuufanya mchakato wa uchaguzi unakubalika.

Wagombea wawili wajitangaza washindi katika duru ya pili ya uchaguzi, Ashraf Ghani (kushoto), na Abdullah Abdullah (kulia.).
Wagombea wawili wajitangaza washindi katika duru ya pili ya uchaguzi, Ashraf Ghani (kushoto), na Abdullah Abdullah (kulia.). AFP Photo/Wakil KOHSAR

Obama amesema hakuna sababu zozote za kulitumbukiza taifa hilo katika dimbwi la machafuko na kutekeleza mambo yalio kinyume na katika na iwapo hali hiyo itatokea, Marekani itasitisha mara moja msaada wake kwa Afghanistan.

Kulingana na matokeo ya muda ya uchaguzi wa urais katika duru ya pili nchini Afghanistan, Abdullah Abdullah ameshindwa kwa asilimia kubwa na mshindani wake Ashraf Ghani, lakini tayari amejitangaza kuwa mshindi na kutupilia mbali matokeo hayo ya muda yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi IEC .

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,  John Kerry.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, John Kerry. REUTERS/Larry Downing

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anatarajiwa kuwasili jijini Kaboul Ijumaa hii kujaribu kuwashawishi viongozi hao na kuokowa taifa hilo kutotumbukia katika machafuko baina ya watu wa kabila la Tadjiks eneo la Kaskazini na ambao wanamuunga mkono Abdullah Abdullah na watu wa kabila la Pachkoune Kusini na mashariki wanaomuunga mkono Ashraf Ghani.