BOLIVIA-UN-ISRAELI-Ugaidi-Usalama

Bolivia yaiweka Israeli kwenye orodha ya mataifa “gaidi”

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, akilani mashambulizi ya jeshi la Israeli dhidi ya shule ya Umoja wa Mataifa katika kijiji cha Jabaliya.
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, akilani mashambulizi ya jeshi la Israeli dhidi ya shule ya Umoja wa Mataifa katika kijiji cha Jabaliya. REUTERS/Eduardo Munoz

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi mapya ya jeshi la anga la Israeli dhidi ya majengo ya Umoja huo ikiwa ni pamoja na makazi, shule na ofisi zake katika ukanda wa Gaza.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari jumatano wiki hii, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, Valerie Amos, ameshutumu mashambulizi hayo na kuyazungumzia kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema mashambulizi ya Israeli dhidi ya shule la Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha vifo vya watu 16 jumatano wiki hii hayaeleweki. Umoja wa Mataifa unaituhumu Israeli kwamba imetekeleza mashambulizi hayo licha ya kuwa ilionywa kwamba shule hilo limewapa hifadhi raia wa kawaida, wala siyo wapiganaji wa Hamas. Wakatai huo huo nchi ya Bolivia imeiweka Israeli kwenye orodha ya mataifa “gaidi”.

Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amethibitisha kwamba , ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Palestina UNRWA ililithibitisha jeshi la Israeli mara 17 kwamba raia waliopewa hifadhi katika shule hilo la Umoja wa Mataifa la Jabaliya ni wakimbizi wa kawaida kutoka Gaza.

“Nashindwa hata kuongea kutokana na yaliyokea katika shule hilo, nabigwa nabutwaa”, amesema Eliasson.

Wapalestina zaidi ya mia moja waliuawa kwa siku ya jana jumatano, na kutimiza idadi ya watu 1.363 ambao wameuawa katika ukanda wa Gaza.

Mkuu wa misaada ya kibinadamu, John Ging, amesema hakubaliani na taarifa zinazosema kwamba kuna mabomu yaliyokua yamefichwa katika shule hiyo. Mabomu yalipatikana katika majengo peke ya Umoja wa Mataifa, baada ya ofisi zake kufungwa kutokana na mapigano, wala siyo katika shule linalowapa hifadhi wakimbizi, ambalo linamilikiwa na Umoja wa Mataifa”, amesema Ging

■  Bolivia imeiweka Israeli kwenye orodha ya mataifa ya “kigaidi”

Rais wa Bolivia, Evo Morales, akiinyooshea kidole Israeli kutekeleza mauaji ya kimbari, akisema Israeli ni nchi "gaidi".
Rais wa Bolivia, Evo Morales, akiinyooshea kidole Israeli kutekeleza mauaji ya kimbari, akisema Israeli ni nchi "gaidi". REUTERS/David Mercado

Baada ya uamzi uliyochukuliwa na Salvador, Peru, Equador na Chile, wa kuwataka mabalozi wake kuondoka nchini Israeli, hatimaye Bolivia imechukua hatua dhidi ya serikali ya Israeli kutokana na mashambulizi ya kijeshi inayoendelea kutekeleza katika ukanda wa Gaza. Rais wa Bolivia, Evo Morales ametangaza jumatano wiki hii kuwa ameiweka israeli kwenye orodha ya mataifa “gaidi”

Juma liliyopita, Bolivia, iliomba Umoja wa Mataifa kuichukulia vikwazo Israeli na kuitaka kusitisha mauaji ya kimbari inayoendelea kutekeleza dhidi ya raia wa Palestina. Mwaka 2009, Bolivia ilivunja uhusiano wake wakidiplomasia na Israeli kutokana na hali kama hiyo.