IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq: Marekani iko tayari kuanzisha mashambulizi katika maeneo yanayo shikiliwa na waasi

Barack Obama akizungumza kuhusu uwezekano wa kufanya mashambulizi katika kwenye ngome za waasi nchini Iraq.
Barack Obama akizungumza kuhusu uwezekano wa kufanya mashambulizi katika kwenye ngome za waasi nchini Iraq. REUTERS/Larry Downing

Marekani imeanzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Irak, baada ya waasi wa nchi hiyo, ambao ni wanamgambo wakislamu kuendelea kuyateka baadhi ya maeneo yaliyokua kwenye himaya ya jeshi la serkali, yakiwemo maeneo yaliyokua yakikaliwa na wakristo.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ambayo, kwa mujibu wa ikulu ya Marekani, ni ya “ kiutu”, kuna uwezekano jershi la anga liendeshe mashambulizi kwenye ngome za wanamgambo hao.

Hata hivo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linatiwa hofu na kuendelea kwa mapigano nchini Iraq, hasa kutimuliwa kwa wakristo katika makaazi yao.

Rais wa Marekani Barack Obama ijumaa wiki hii ameagiza ndege zake za kijeshi kurejea nchini Iraq kudondosha chakula cha msaada kwa raia wanaokimbia makazi yao na ikiwezekana kutekeleza mashambulizi ya anga katika kile alichodai kunusuru kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Rais Obama amesema kuwa ndege hizo zitashambulia ngome za wapiganaji wa kundi hilo iwapo watajaribu kusonga mbele kuelekea mji wa Arbil ambako Marekani ina maofisa wake.

Jeshi la Marekani limethibitisha kwamba limepewa amri ya kutekeleza mashambulizi, lakini mashambulizi hayo hayajaanza. Jeshi hilo limebaini kwamba ndege za Marekani zimeanza kudondosha chakula na misaada mingine ya kiutu katika jimbo la Kurdistan nchini Iraq, ambako wakristo walikimbila

Ni kwa mara ya kwanza toka kutangaza kuondoa majeshi yake nchini Iraq mwaka mmoja uliopita, serikali ya Marekani kutangaza operesheni mpya inayolenga kusaidia utawala wa Iraq kukabiliana na waasi wa kiislamu wa Islamic State.

Balozi wa Iraq kwenye Umoja wa Mataifa, Mohammed Ali Al-Hakim, hata hivo amethibitisha kuweko kwa mazungumzo kati ya Washington na Baghdad kuhusu uwezekano wa jeshi la Marekani kutekeleza mashambulizi kwenye ngome za wanamgambo wa kislamu.