PALESTINA-ISRAELI-MAREKANI-HAMAS-Uchumi

Palestina: Gaza: mapigano yarindima

REUTERS/ Amir Cohen

Jeshi la Israeli limetangaza ijumaa kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya Hamas baada ya makombora kurushwa kwenye ardhi ya Israel usiku wa kuamkia leo, maroketi ambayo jeshi la Israel limesema kuwa yalirushwa na wapiganaji wa kundi la Hamas, baada ya kumalizika muda wa siku tatu wa kusitisha mapigano.

Matangazo ya kibiashara

“Mapema leo asubuhi, baada ya kurushwa kwa makombora katika aridhi ya Israel, jeshi limeendesha mashambulizi ya kuvizia kwenye ngome za magaidi katika ukanda wa Gaza”, jeshi la Israel limesema katiak tangazo lililotoa, saa chache kabla ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kutoa amri ya kujibu kwa mashambulizi kufuatia kitendo cha Hamas cha kurusha makombora katika aridhi ya Israel.

Kwenye mtandao wake wa Twitter jeshi la Israel limelituhumu kundi la Hamas kwa kutekeleza shambulio hili licha ya hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa na utawala wa Tel-Aviv ikiwemo uwezekano wa kuongeza muda zaidi wa kusitisha mapigano.

Jeshi la Israeli limetekeleza mashambulizi ya anga, huku likitumia vifaru kwa kurusha makombora katika ukanda wa Gaza, bila hata hivo kuwepo na vikosi vya aridhini katika aridhi ya Gaza, amesema msemaji wa jeshi, lakini mashuhuda wamesema wamesema jeshi la Israeli limetekeleza mashambulizi ya anga kaskazini na katikati ya ukanda wa Gaza.

Rais Obama amesisitiza nchi yake kuendelea kuiunga mkono Israel dhidi ya mashambulizi ya Hamas, na kwamba hana huruma yoyote kwa kundi hilo.

Haya yanajiri wakati huu ambapo mazungumzo kati ya Israel na viongozi wa mamlaka ya palestina yakiendelea mjini Cairo Misri.