MAREKANI-IRAQ-Siasa

Marekani : Barack Obama apongeza uteuzi wa waziri mpya wa Iraq

Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza hatua ya kuteuliwa kwa aliyekuwa naibu spika wa bunge Haidar al Abadin kuwa waziri mkuu mpya nchini Iraq.

Rais wa Marekani Barack Obama, akipongeza ueteuzi wa Haidar al Abadin kuwa waziri mkuu mpya nchini Iraq.
Rais wa Marekani Barack Obama, akipongeza ueteuzi wa Haidar al Abadin kuwa waziri mkuu mpya nchini Iraq. REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ambayo ililenga pia kutowa ujumbe kwa waziri mkuu alieondolewa madarakani licha ya kutomtaja moja kwa moja na ambaye ameonyesha nia ya kutoachia madaraka.

Akizungumza akiwa katika kisiwa cha Martha's Vineyard katika jimbo la Massachusetts kaskazini mashariki ambako yupo likizo na familia yake, Obama amefahamisha kwamba ameahidi Kumuunga mkono waziri mkuu huyo mpya Haïdar al-Abadin na amewatolea wito viongozi wote wa kisiasa nchini Irak kufanyakazi kwa mshikamano.

Rais Obama amesisitiza kuhusu hatuwa ya kuunda baraza la mawaziri haraka iwezekanavyo itayo shirikisha pande zote kwa manufaa ya wananchi wote wa Irak na ambayo itapambana na kundi la wapiganaji wa kiislam la Isil.

Nouri al-Maliki,waziri mkuu wa Iraq aliyetimuliwa madarakani.
Nouri al-Maliki,waziri mkuu wa Iraq aliyetimuliwa madarakani. REUTERS/Mushtaq Muhammed

Jumatatu wiki hii waziri mkuu wa zamani Nouri Al Malik ambaye utawala wake umekuwa ukikosolewa vikali na Marekani tangu kipindi kadhaa, amemtuhumu rais wa nchi hiyo kwa kuvunja katiba baada ya kuchukuwa hatuwa ya kumteuwa waziri mkuu mpya wakati muhula wake bado haujatamatika.