Iraq: ISIS yakabiliwa na mashambulizi ya Marekani
Imechapishwa:
Marekani imeanza mashambulizi mapya dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa ISIS nchini Iraq katika miji ya Mosul Dam na Amerli.
Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon inasema ndege zake za kivita zimefanikiwa kuharibu magari ya wapiganaji wa ISIS karibu na mji wa Mosul Dam.
Licha ya kujaribu kuliangamiza kundi hili, Marekani imesema mashambulizi haya pia yamesaidia ili msaada wa kibiandamu uwafikie wanajeshi wa Iarq wanaopambana na wapiganaji hawa ambao wamejihami vilivyo.
Hadi sasa Marekani imetekeleza mashambulizi ya anga 120 dhidi ya wapiganaji wa kiislam ambao imesema ni hatari na haijawahi kuona kundi lililojihami kwa silaha hatari kama ISIS.
Makabiliano haya pia yamesabisha raia wengi kukimbia makwao na wakaazi wa Amerli hawana chakula na wale wanahofia maisha yao kwa kile wanachodai ni Washia.