MAREKANI-SYRIA-IRAQ-ISIL-Usalama-Haki za binadamu

Raia wa pili wa Marekani aliekua akishikiliwa mateka auawa

Mmoja wa wajumbe wa taifa la kiislam akishikilia bendera ya wapiganaji wa kiislam katika mji wa Racca nchini Syria baada ya kutangazwa mkuu wa taifa la kiislamu (Khalifa).
Mmoja wa wajumbe wa taifa la kiislam akishikilia bendera ya wapiganaji wa kiislam katika mji wa Racca nchini Syria baada ya kutangazwa mkuu wa taifa la kiislamu (Khalifa). REUTERS/Stringer

Wapiganaji wa Kiislamu nchini Iraq wametoa mkanda wa video unaonesha kuuliwa kwa kukatwa kichwa kwa mwanahabari mwingine wa Marekani Steven Sotloff ambaye amekuwa mikononi mwa wapiganaji hao.

Matangazo ya kibiashara

Sotloff mwenye umri wa miaka 31 alitekwa nyara nchini Syria mwaka 2013 akiwa kazini, na mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni mwezi uliopita akiwa na mwandishi mwingine wa Marekani James Foley ambaye pia aliuawa kwa kukatwa kichwa na wapiganaji hao.
Msemaji wa rais Barrack Obama, Josh Earnest amesema maafisa wa Inteljensia wanachunguza uhalali wa mkanda huo.

Wapiganaji hao wa IS walitishia kumuua mwanahabari huyo ikiwa Marekani itaendelea kuwashmabulia katika ngime zao.

Idadi ya raia wa kigeni wanaoshikiliwa mateka na wapiganaji wa kiislamu haijulikani, lakini inasadikiwa kuwa kati ya 50 na 60, wakiwemo wanahabari 20. Mapardri na maaskofu ni miongoni mwa mateka hao wanaoshikiliwa na wapiganaji wa kiislam.

Baadhi ya wanahabari walitekwa nyara baada ya kunyooshewa kidole na wakalimani wao aidha madereva wao.

MatthewShrier, mpiga picha, raia wa Marekani ambaye alifaulu kutoroka baada ya kushikiliwa mateka na wapiganaji hao wa kiislam mwezi Agosti mwaka 2013, amebaini kwamba aliziwiliwa akiwa pamoja na watu wengine 22 katika vyumba mbali mbali vya jengo moja linalodhaniwa kama "kiwanda cha mateka", huku akibaini kwamba mateka walikua wakizuiliwa katika vyumba kulingana na uraia wao.