MAREKANI-UN-SYRIA-IS-Usalama

Obama apongeza mashambulizi ya Marekani Syria

Ndege mbili za kivita za Marekani zenye chapa F/A-18E Super Hornet ni miongoni mwa ndege zitakazotumiwa katika mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Ndege mbili za kivita za Marekani zenye chapa F/A-18E Super Hornet ni miongoni mwa ndege zitakazotumiwa katika mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam. REUTERS/U.S. Navy

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na marekani na washirika wake wa nchi za kiarabu nchini Syria yameanza kwa mafanikio na yanatuma ujumbe kwa wapiganaji wa kijihadi kuwa dunia imeungana ili kukabiliana nao.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hioyo ya Rais Obama inakuja siku moja baada ya kuanza kwa operesheni ya mashambulizi ya anga nchini Syria huku marekani ikidai kuwa inawelenga wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic state.

Katika mashambulizi hayo imeelezwa na marekani kuwa wapiganaji wengi wa kundi la Islamic State na kundi la kigaidi la Al Qaeda wameuawa na wataendelea kuwalenga magaidi hao ambao wamekuwa wakipanga kufanya mashambulizi katika nchi za magharibi.

Rais obama amezishukuru nchi washirika kwa kuunganisha nguvu ili kukabiliana na magaidi ambao wanatishia usalama wa kanda ya mashariki ya kati na dunia kwa ujumla.

Rais huyo wa Marekani amepongeza operesheni inayoendeshwa na jeshi lake nchini Syria dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa hakutakua na njia salama ya kuwalinda raia kama makundi ya wapiganaji wa kijihadi hayataangamizwa.

“ Kuhusu suala la Syria, hakutakua na njia sahihi ya kutoa ulinzi kwa raia wa Syria iwapo hakutakua na jitihada madhubuti ya kuwasambaratisha wapiganaji wa kijihadi na kuachwa waendelee kufanya mauaji”, amesema Ban K-moon, huku akibaini kwamba raia wa Syria hawawezi kuwa salama kama serikali ya Sanaaitaendelea kufanya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wake.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa mashambulizi hayo dhidi ya wapiganaji wa kijihadi yanayoongozwa na marekani yanaweza kusaidia kupunguza vitendo vya kigaidi vinavyotishia usalama wa dunia inawaje marekani hapa inaonyesha sura mbili kama anavyoeleza.