AFGHANISTAN-USALAMA

Watu wanne wapoteza maisha wakati rais mpya akiapishwa nchini Afghanistani

Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani kulia na waziri mkuu Abdullah abdullah waziri mkuu kushoto wakati wa kula kiapo
Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani kulia na waziri mkuu Abdullah abdullah waziri mkuu kushoto wakati wa kula kiapo AFP PHOTO/SHAH Marai

Watu watatu wamepoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Taliban mapema leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa jijini Kaboul licha ulinzi mkali wakati huu rais mpya wa nchi hiyo Ashraf Ghani akiapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa Taliban ambao wametolewa wito wa mazungumzo na serikali wamejigamba kuhusika katika shambulio hilo kupitia msemaji wake Zabiullah Mujahid.

Katika hotuba yake Ashra Ghani amewatolea wito wa amani wapiganaji wa Taliban wakati akimrithi rasi Hamid Karzai alieongoza nchi hiyo tangu mwaka 2001 wakati mataifa ya magharibi yalipoingilia kati kijeshi nchini humo, ikiwa ni hatuwa ya kihistoria ya ubadilishanani madaraka kwa misingi ya kidemokrasia katika nchi hiyo yenye kukumbwa na machafuko wakati huu vikosi vya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi Nato vikijiandaa kuondoka nchini humo.

Ashraf Ghani, rais mpya wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 65 mchumi
Ashraf Ghani, rais mpya wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 65 mchumi REUTERS/Omar Sobhani

Wakati akikabidhi madaraka, rais Karzai amesema amejawa na furaha kupeana madaraka na mrithi wake baada ya kuwa kwenye uongozi kwa kipindi cha Miaka 13 huku nchi hiyo ikikumbwa na vita katiya majeshi ya Marekani na wapiganaji wa Taliban.

Rais Mpya ametumia fursa hiyo kwa kuwatolea wito wapizani hususan wapiganaji wa Taliban pamoja na wapiganaji wa kundi la Hezb-e-Islam kuanzisha mazungumzo ya kisiasa na serikali mpya. Ghani mwenye umri wa miaka 65 mfanyakazi zamani wa benki kuu ya dunia na waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya kwanza ya Rais Karzai.

Ghani amesema kwa vyovyote vile, suluhu lazima ipatikane, na kuwataka wanabijiji kudai amani na kutowa wito kwa viongozi wa kidini, ma Imam ili wawashawishi wapiganaji wa Taliban na kuachana nao iwapo hawatowasilikiza. Ameendelea kusisitiza Ashraf Ghani ambaye amepokelewa kwa shambulio la kujitowa muhanga.

Kulingana na msemaji wa polisi, mshambuliaji wa kujitowa muhanga amejilipua katika uwanja wa ndege wa mjini Kaboul na kuwauwa watu wanne na wengine wawili wamejeruhiwa wakati ambapo kulikuwa na ulinzi mkali huku wajumbe kutoka Marekani, China, India na Pakistan walipokuwa wakiwasili kuhudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa rais Ghani.

Rais Ashraf Ghani kati, makam wa kwanza wa rais Abdul Rashid Dostum kushoto na makam wa pili wa rais  Sarwar Danish  29.9.2014.
Rais Ashraf Ghani kati, makam wa kwanza wa rais Abdul Rashid Dostum kushoto na makam wa pili wa rais Sarwar Danish 29.9.2014. REUTERS/Omar Sobhani

Kulingana na msemaji wa Tlaiban Zabiullah Mujahid, mashambulizi hayo yalilenga wanajeshi wa kigeni na wale wa nchi hiyo.

Mra kadhaa rais Karzai amewatolea wito wa Taliban kwa mazungumzo ya amani ili kurejesha utulivu katika nchi hiyo wakati huu vikosi vya Nato vikijiandaa kuondoka nchini humo mwakani. Wito ambao umekuwa ukitupiliwa mbali na wapiganaji hao ambao wanamtuhumu Karzai kuwa kibaraka wa serikali ya Marekani. Hivi karibuni wapiganaji wa Taliban wametathmini rais mpya wa nchi hiyo Ashraf Ghani na kumuona kuwa kibaraka pia wa Marekani, hali inayo tia wasi wasi kuendelea kuhshuhudia uhusiano mbaya kati ya serikali na kundi hilo.