MAREKANI - AFYA

Mgonjwa wa kwanza wa Ebola aripotiwa nchini Marekani

Hospital ya Texas Health Presbyterian Hospital,
Hospital ya Texas Health Presbyterian Hospital,

Marekani imethibitisha maambukizi ya kwanza ya Ugonjwa hatari wa Ebola katika jimbo la Texas. Msemaji wa kituo cha Afya cha udhibiti wa maradhi amearifu hapo jana Septemba 30. hadi sasa mtu huyo hajatambulika, na haijulikani ajira yake, lakini hivi karibuni alisafiri nchini Liberia na amelazwa katika Hospital ya Dallas. Liberia ni miongoni mwa nchi zilizo guswa sana na maradhi haya ya Ebola. 

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya iliotolewa na Hospital ya Texas Health Presbyterian Hospital, Mtu huyo amewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia kuonyesha dalili za Ebola na safari aliyo ifanya hivi karibuni nchini Liberia.

Mgonjwa huyo alirejea nchini Marekani akitokea Liberia Septemba 20. viongozi wa Hospital hiyo wanasema alianza kuonyesha dalili za Ebola siku kadhaa baada ya kuwasili jijini Texas na amewekwa katika hali ya tahadhari tangu Septemba 26.

Wahudumu wa afya katika jimbo hilo wanasema, mgonjwa huyo ambaye hajatajwa jina ametengwa na watu wengine na anapewa matibabu.

Inaelezwa kuwa mtu huyo aliambukizwa Ebola nchini Liberia, kabla ya kusafiri nchini Marekani na wakati wa safari yake wiki mbili zilizopita, hakuonesha dalili zozote za kuwa na Ebola.

Marekani imekuwa katika mstari wa mbele kupambana na Ebola katika nchi za Afrika Magharibi na imetuma wanajeshi wake zaidi ya elfu tatu katika nchi hizo kusaidia kupambana na uginjwa huo.

Hadi kufikia sasa, Shirika la afya duniani linasema zaidi ay watu elfu 3 wamepoteza maisha katika nchi za Afrika Magharibi.