MAREKANI-SYRIA-IRAQ-ISIL-Usalama-Haki za binadamu

Marekani: vita dhidi ya IS vinaweza kudumu miaka 30

Leon Panetta, Waziri wazamani wa ulinzi wa Marekani.
Leon Panetta, Waziri wazamani wa ulinzi wa Marekani. DR

Waziri wa zamani wa ulinzi katika utawala wa barack Obama, Leon Panetta ameandika kitabu ambamo anautuhumu utawala wa Obama kwa kuanzisha vita dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiisalam, akibaini kwamba Marekani imejitangazia vita dhidi ya makundi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Leon Panetta, ambaye aliwahi kua pia mkuu wa Idara ya ujasusi ya Marekani amekemea vikali utaratibu unaotumiwa na rais Obama dhidi ya ugaidi nchini Iraq na Syria, akisema vita hivyo vitachangia kwa kukuza machafuko yatakayodumu miaka 30.

Wakati mapigano yakiendelea kurindima nchini Syria, huku wapiganaji wa Dola la Kiislamu wakiendelea kupambana na muungano wa kimataifa, Leon Panetta ametoa kauli nzito ambayo imeikwaza Ikulu ya washington.

Leon Panetaa, amesema Barack Obama “ ameanzisha vita nchini Syria na Iraq dhidi ya wapiganaji wa dola la Kiislam kwa maslahi ya taifa lake”, na hali hiyo haitaendelea kusalia hivo katika nyoyo za wengi. Kauli hiyo kwa sasa ndio inagonga vichwa kwenye mitandao yote ya kijamii.

“ Nadhani kwamba tunaingia katika vita vitakavyodumu miaka 30, kunahitajika muda wa kutosha ili kuendesha vita dhidi ya makundi hayo... Na kama tungelianzisha vita hivyo, miaka miwili iliyopia, tungelikua kwenye nafasi nzuri”, Leon Panetta ameandika kwenye kitabu chake alichokiita “Worthy Fights” ikimaanisha “vita vinavyotakiwa kuendeshwa”.

Mkuu huyo wa zamani wa Idara ya ujasusi ya Marekani, ameelezea masikitiko yake kuona rais Barack Obama amekua akichukua uamzi bila hata hivo kuendesha uchunguzi wa kina.

Kwa upande wake, msemaji wa Ikulu ya Washington, ameelezea masikitiko yake kuona mtu ambaye alipewa na Barack Obama majukumu ya kushikilia nyadhifa nuhimu nchini anatoa kauli hiyo.