CANADA-Usalama

Shambulio katika mji wa Ottawa: “Canada haitokubali kutishwa”

Waziri mkuu wa Canada Stephen Harper wakati akilihutubia taifa baada ya tukio hilo kutokea, Jumatano Oktoba 22 mwaka 2014.
Waziri mkuu wa Canada Stephen Harper wakati akilihutubia taifa baada ya tukio hilo kutokea, Jumatano Oktoba 22 mwaka 2014. REUTERS/CBC/Pool

Waziri mkuu wa Canada Stephen Harper amesema mtu alieshambulia Bunge la taifa katikamji wa Ottawa na kumuuwa mwanajeshi mmoja wa serikali kabla ya kuauwa, ni tukio la kigaidi. Mtu huyo alizua mtafaruku Jumatano Oktoba 22 bungeni kwa kushambulia kwa risase.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wawilii wameuawa nchini Canada katika kipindi cha siku tatu. Mtu anaye julikana kwa jina la Michael Zehaf-Bibeau mwenye umri wa miaka 32 alizua mtafaruku Jumatano Oktoba 22 nchini Canada kwa kuendesha shambulizi Bungeni, na kumuua mwanajeshi mmoja, kabla ya kuuawa na polisi hali ambayo ilizua hofu kubwa kwa polisi waliozingira eneo la makaazi ya Bunge wakihofia huenda wapo wahalifu wengine.

Mea wa jiji la Ottawa Jim Watson amethibitisha kwamba polisi wameondowa vizuizi katika eneo hilo baada ya kupata uhakika kwamba mshambuliaji huyo alikuwa pekeake.

Inasadikiwa pia kuwa kuna uhusiano kati ya tukio hili na lile lililotokea mwanzoni mwa juma hili katika kitongoji cha jiji la Montreal ambapo mwajaeshi mwingine aliuawa kwa kugongwa na gari. Mtu huyo aliejulikana kwa jina la Martin Rouleau-Couture, aliesilimu hivi karibuni na ambaye anaunga mkono itikadi za kijihadi alikuwa miongoni mwa vijana 90 wanaoshukiwa kupanga njama za kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Canada.

Serikali ya Canada imesema tukio hilo ni la kigaidi ikiwa ni tukio la kwanza kabisa la Kigaidi kufanyika nchini humo.

Serikali ya Ottawa imetowa wito kwa wananchi wake kuwa wangalifu zaidi katika kipindi hiki ambacho kunahofu ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi baada ya nchi hiyo kujiunga na vikosi vya muungano unaongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, ambalo linadhibiti baadhi ya maeneo katika nchi ya Iraq na Syria.