MAREKANI-EBOLA-Afya

Ebola: Barack Obama awahakikishia raia wa Marekani

Rais wa Marekani akizungumza kuhusu Ebola, kwenye Ikulu ya Wachington, Jumanne Oktoba 28.
Rais wa Marekani akizungumza kuhusu Ebola, kwenye Ikulu ya Wachington, Jumanne Oktoba 28. REUTERS/Kevin Lamarque

Hakuna mtu anaye ripotiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Marekani, baada ya ugonjwa huo kudhibitiwa vilivyo. Daktari mmoja na wauguzi wa wili waliyoambukizwa hivi karibu virusi vya Ebola walipona. Muuguzi wa mwisho aliruhusiwa kuondoka hospitali Jumanne Oktoba 28.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku kadhaa ya hofu, hatimaye rais wa Marekani, Barack Obama ametolea wito raia Jumanne Oktoba 28, akiwahakikishia kwamba ugonjwa huo umedhibitiwa na hakuna mtu yeyote anaye ripotiwa na ugonjwa huo katika ardhi ya Marekani.

Asilimia kati ya 60 na 70 ya raia wa Marekani wana hofu ya maabukizi ya virusi vya Ebola, kulingana na uchunguzi uliyoendeshwa hivi karibuni. Hata hivo, Barack Obama amesema kwa jumla ya watu 10 waliyofanyiwa uchunguzi wauguzi wa waili ndio walibainika kuwa na virusi vya Ebola katika ardhi ya Marekani, lakini kwa sasa wauguzi hao wamepona, ameseama rais Obama.

Kuona rais wa Marekani akilazimika kuzungumza kuhusu mlipuko huu wa Ebola, inaonyesha kiwango cha wasiwasi kinachotokana na uvumi wa kila aina.

Wakati huu kunashuhudiwa mvutano nchini Marekani kati ya viongozi wa serikali za mitaa na wanasayansi. Madaktari, wauguzi na watafiti walipongezwa hivi karibuni na rais Barack Obama: "Hatutaki kukata tamaa wafanyakazi wa afya ambao wamekua mstari wa mbele kwa kujaribu kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Ebola dhidi ya Afya yetu ! Kwa sababu wakikusanyika kwa pamoja hatutokua na wasiwasi kuhusu Ebola hapa Marekani".