APEC-MAREKANI-CHINA-SOKO-UCHUMI-Diplomasia

Mkutano wa Apec Beijing: Obama aipongeza China

Rais wa Marekani, Barack Obama wakati wa hotuba yake katika mkutano wa kilele wa Apec Pekin, Novemba 2014.
Rais wa Marekani, Barack Obama wakati wa hotuba yake katika mkutano wa kilele wa Apec Pekin, Novemba 2014. MANDEL NGAN / AFP

Hotuba ya Barack Obama imegubikwa na maneno makali dhidi ya nchi 20 zinazoshiriki tangu Jumatatu Novemba 10 mkutano wa kilele wa Apec.

Matangazo ya kibiashara

China ni mshirika wa kiuchumi wa nguvu kwa Marekani, lakini rais wa Marekani hakuzungumzia jambo la kuvutia, ispokua kuitolea wito China kuheshimu haki za binadamu.

"Ni dhahiri Marekani ni taifa la Ukanda wa Pasifiki," Obama amesema, huku akipigiwa makofi. "Maisha yetu, usalama na ustawi wetu ni miongoni mwa mambo ambayo yanahusishwa na Asia! ", ameongeza rais wa Marekani.

Ikiwa na asilimia 60 ya utajiri duniani pamoja na watu bilioni 3 wanaotumia bidhaa zake, rais Obama anaona Asia kama "nafasi ya ajabu kwa kujenga ajira nchini Marekani. Na miongoni mwa mataifa ya Asia, mshirika anaeongoza kwa raia wa Marekani ni China”, amesema rais Obama. Lakini Washington inaitaka Beijing kuweka sawa soko lake huria na ubadilishaji wa sarafu yake.

"Kama tutashirikiana pamoja, dunia itafaidika," amesema Barack Obama. "Tunaipongeza China, amani na utulivu na mafanikio ya China", ameendelea kusema Obama. Washington inataka changamoto ya kimataifa na Beijing, kama vile ugaidi wa kimataifa, mapambano dhidi ya Ebola au mabadiliko ya hali ya hewa.

Barack Obama ameelezea mambo muhimu mwishoni mwa hotuba yake, ambapo ameitolea wito Beijing kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari: "Hatuiombi China iufuate mfano wa Marekani katika nyanja zote. Lakini tutaendelea kutiwa wasiwasi kuhusu haki za binadamu kwa namna zinavyoendelea kuvunjwa" amesema Obama.