ISRAELI-PALESTINA-JORDAN-MAREKANI-Suluhu-Usalama

Mapigano Jerusalem: Kerry, Netanyahu na Mfalme Abdullah II wakutana

Mfalme wa Jordan, Abdallah II akimpokea kwa mazungumzo katika Kasri lake Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Amman Novemba 13 mwaka 2014.
Mfalme wa Jordan, Abdallah II akimpokea kwa mazungumzo katika Kasri lake Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Amman Novemba 13 mwaka 2014. REUTERS/Muhammad Hamed

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, John Kerry, waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu pamoja na mfalme wa Jordan, Abdallah II wamekutana kwa mazungumzo Alhamisi jioni Novemba 13 katika mji wa Amman ili kujadili kuhusu kuengezeka kwa mashafuko Jerusalem Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Machafuko yanayoendelea kushuhudiwa Jerusalem Mashariki yameanza kuuaathiri mji mkuu wa Israel. Maeneo yanayokaliwa na jamii ya Warabu yamekua yakiteketea kwa moto, jambo ambalo Netanyahu anatakiwa kupatia suluhu haraka iwezekanavyo ili kurejesha utulivu katika mji mtakatifu na maeneo mengine yanayo kaliwa na Warabu.

Mfalme wa Jordan, Abdalallah II, ambae nchi yake ndio inatoa ulinzi wa Mskiti mtakatifu wa Al-Aqsa, ametupilia mbali kile alichokiita uvamizi na uchokozi wa kila mara unofanywa na mjini Jerusalem hasa katika Msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa.

Kabla ya mkutano huo, mfalme Abdallah alimpokea kwa mazungumzo rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa kuna hatua kubwa zilizofikiwa katika mazungumzo yake na serikali ya Israel na Palestina hatua ambazo zitasaidia kupunguza mtikisiko katika mgogoro wa pande hizo mbili.

John Kerry ametoa kauli hiyo baada ya kufanya mazungumzo na Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu pamoja na mfalme wa Jordan Abdullah II na hivyo kuondoa wasiwasi wa kutofikiwa kwa maeneo ya hija mashariki mwa Jerusalem.

John Kerry amesema kuwa pande zote zinaguswa na umuhimu wa upatikanaji amani ikiwemo Israeli, na kwamba hatua hizo zilizofikiwa ni muhimu katika kumaliza mapigano ambayo yamekuwa yakizuka mara kwa mara.