MAREKANI-CUBA-DIPLOMASIA

Marekani yaondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya Cuba

Raia wa Marekani wameruhusiwa kuingia Cuba na kuanzisha biashara, kushiriki katika kubadilishana utamaduni, utafiti, ujumbe wa kibinadamu na semina mbalimbali.
Raia wa Marekani wameruhusiwa kuingia Cuba na kuanzisha biashara, kushiriki katika kubadilishana utamaduni, utafiti, ujumbe wa kibinadamu na semina mbalimbali. REUTERS/Stringer

Marekani imelegeza vikwazo vya kusafiri na biashara ilivyokua iliiwekea Cuba, kufuatia kuachiliwa huru kwa wafungwa 53 wa kisiasa, uamzi uliyochukuliwa na serikali ya Cuba.

Matangazo ya kibiashara

Hatua zilizotangazwa na Washington zimeanza kutekelezwa leo Ijumaa Januari 16. Hatua hizi zinafuatia tangazo lilotolewa na Barack Obama, Desemba 17. Vikwazo viliyochuliwa Cuba vinadumu zaidi ya miaka 50 sasa.

Licha ya hatua hizo, bado kunasubiriwa kura ya Baraza la Wawakilishi ili vikwazo viliyochukuliwa dhidi ya Cuba viondolewe. Hata hivyo masuala ya biashara yamerahisishwa kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Anne-Marie Capomaccio, madhumuni ya hatua ya kwanza iliyotangazwa na Washington itawezesha kukuza biashara kati ya raia wa kawaida wa Cuba na sekta ya kibinafsi, ambayo imezinduliwa tangu kuwasili madarakani kwa Raul Castro.

Mbali na mahusiano ya kifamilia, sekta mbili zimepewa kipaumbele. Sekta hizo ni pamoja na mawasiliano ya simu na kila kitu kinachohusiana pamoja na Intaneti na kompyuta.

Wizara ya fedha ya Marekani pamoja na Ikulu ya Washington zimezingatia sekta hizo muhimu. Inaeleweka kwamba lengo la Marekani ni kuhimiza uhuru zaidi wa mawasiliano na habari kwa ajili ya raia Cuba.

Tangu sasa raia wa Marekani ameruhusiwa kuingia Cuba na kuanzisha biashara, kushiriki katika kubadilishana utamaduni, utafiti, ujumbe wa kibinadamu na semina mbalimbali.