SWISSLEAKS-UTAJIRI-UCHUMI

Kesi ya SwissLeaks hadi Amerika ya Kusini

Nchi ya Venezuela, moja ya nchi za Amerika ya Kusini inaongoza kwa watu wanowekeza katika benki ya Uswisi ya HSBC ikiwa na kitita cha Yuro bilioni 13.
Nchi ya Venezuela, moja ya nchi za Amerika ya Kusini inaongoza kwa watu wanowekeza katika benki ya Uswisi ya HSBC ikiwa na kitita cha Yuro bilioni 13. REUTERS/Jorge Silva

Mawimbi ya uchunguzi wa kesi ya SwissLeaks yamevuka bahari Atlantiki na kufikia Amerika ya Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa, wanamichezo au wawekezaji, na watu wengine wengi wamefanyiwa uchunguzi na jarida la Ufaransa Le Monde na shirika la kimataifa la wanahabari wenye taaluma ya uchunguzi, na kugunduliwa kuwa wanawekeza kinyume cha sheria mabilioni ya pesa katika benki ya Uswisi ya SwissLeaks.

Nchi ya Venezuela, moja ya nchi za Amerika ya Kusini inaongoza kwa watu wanowekeza katika benki hiyo ya Uswisi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Quito, Eric Samson, nchi ya Venezuela, Amerika ya Kusini, inaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaowekeza katika benki hiyo ya SwissLeaks.

Takribani Yuro bilioni 13 ziliingia kati ya mwaka 2005 na 2007 katika akaunti ya tawi la benki ya Uswisi inayopatikana katika benki ya Uingereza ya HSBC. Jina la mtu aliyewekeza kitita hicho cha Yuro katika benki hiyo ni Alejandro Andrade, ambaye aliwahi kuwa afisa mlinzi wa rais wa zamani wa Venezuela aliyefariki, Hugo Chavez, na aliwahi kuwa pia mkurugenzi mkuu wa Hazina ya taifa ya Venezuela na benki ya maendeleo ya nchi hiyo.

Brazili imetajwa pia kuwa na idadi kubwa ya watu wanaowekeza katika benki hiyo ya Uswisi ya SwissLeaks. Zaidi ya raia 5000 wa Brazil waliwekeza Yuro bilioni 6, ikiwa ni mara mbili ya wateja kutoka Argentina.

Kwa mujibu wa jarida la kila siku la Nacion de Buenos Aires, mmoja wa wateja wakuu wa benki ya Uingereza ya HSBC inayoshirikiana na SwissLeaks alikuwa mhasibu aitwaye Gerardo Miguel Abadi, meneja wa mfuko wa fedha (Gems inversion).

Nchi ya Uruguay haikuachwa nyuma, ambapo nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya soka, Diego Forlan ametajwa kwenye orodha ya watu wanaowekeza katika benki hiyo.

Nchini Ecuador, muwekezaji tajiri, Alvaro Noboa ndiye anaongoza kwa kuwekeza katika benki hiyo ya HSBC. Tajiri huyo aliwekeza zaidi ya Yuro bilioni 85 kati ya mwaka 2006 na 2007.