ISRAELI-MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Netanyahu atazamiwa kulihutubia Bunge la Congress

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, akiwa ziarani Marekani.
Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, akiwa ziarani Marekani. Reuters/Debbie Hill/Pool

Waziri wa Israel Benjamin Netanyahu amewasili jijini Washington DC nchini Marekani kulihutubia Bunge la Congress kuhusu mradi wa Nyuklia nchini Iran.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Netanyahu anatarajiwa kulihutubia Bunge la Congress Jumanne Machi 3 kuhusu hatari za mradi wa Nyuklia wa Iran kwa taifa lake la Israel.

Ziara hii ya Netanyahu nchini Marekani inakuja wiki mbili kabla ya Uchagizi mkuu nchini Israel na chama cha Netanyahu, Likud kimekuwa kikishuhudia ukosoaji mkubwa nyumbani.

Rais Barrack Obama hajafurahia ujio wa Netanyahu na hotuba anayiotarajiwa kuitoa Jumanne wiki hii, lakini Waziri huyo wa Israel amepata uungwaji mkono kutoka kwa wanasiasa wa Republican ambao walimwalika kulihutubia bunge.

Wiki iliyopita, Netanyahu aliishutumu serikali ya rais Obama na mataifa mengie ya Magharibi kutofanya vya kutosha kuizua Iran kuendelea na mradi wake wa Nyuklia, madai yaliyokanushwa na Waziri wa Mambo ya nje John Kerry.

Marekani imekuwa ikiongoza mazungumzo ya amani kati ya mataifa ya Magharibi na Iran kuhusu mradi huu wa Nyuklia, mazungumzo yanayotarajiwa kufikia mwisho katikati ya mwaka huu.