ISRAELI-MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Hali ya kutoelewana kati Obama na Netanyahu yaendelea

Mahojiano ya kwanza ya Binyamin Netanyahu na Barack Obama katika ofisi moja ya White House Mei 18 mwaka 2009.
Mahojiano ya kwanza ya Binyamin Netanyahu na Barack Obama katika ofisi moja ya White House Mei 18 mwaka 2009. (Photo : Reuters)

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netayahu leo anatarajiwa kulihotubia bunge la Congress nchini Marekani, na kutoa mtazamo wa nchi yake kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu mradi wa Nyuklia nchini Iran.

Matangazo ya kibiashara

Barack Obama na Benjamin Netanyahu wote wawili waliingia madarakani mwaka 2009 na kati yao uhusiano umedorora. Katika hotuba yake mjini Cairo mwaka huo, Rais wa Marekani kwa alitangaza akisisitiza kwamba ukoloni wa Israel kwenye maeneo ya Palestina unapaswa kusitishwa.

Akizungumza Jumatatu wiki hii na Waisraeli wenye uraia wa Marekani, Netanyahu alisema anaiheshimu serikali ya Obama na kusisitiza kuwa Marekani na Israeli haziungi mkono mradi wa Nyuklia nchini Iran lakini wao kama viongozi wanatofautiana kuhusu njia gani ya kutumia ili kuizuia Iran kuendelea na mradi huo.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumza akiwa jijini Geneva nchini Uswizi amemtaka Netanyahu kutogusia yale waliyokubaliana na Iran kuhusu mradi wake, hali ambayo inaweza kusababisha mazungumzo kukwama.

Israel imesema, mpango wa Nyuklia wa Iran unaendelea kutishia usalama wa Israel.