MAREKANI-BROWN-UCHUNGUZI-USALAMA

Uchunguzi kuhusu kifo cha Michael Brown

Wizara ya Sheria nchini Marekani imesema kuwa imetamatisha uchunguzi kuhusu kifo cha kijana mmoja mweusi Michael Brown aliyeuawa mjini Ferguson na kubaini kuwa kulikuwa na viashiria vya ubaguzi wa rangi wakati wa tukio hilo.

Wazazi wa Michaël Brown (Katikati) wakati wa mkutano na vyombo ya habari pamoja na wanaharakati  wa haki za binadamukatika mji wa Ferguson, katika jimbo la Missouri, Novemba 25 mwaka 2014.
Wazazi wa Michaël Brown (Katikati) wakati wa mkutano na vyombo ya habari pamoja na wanaharakati wa haki za binadamukatika mji wa Ferguson, katika jimbo la Missouri, Novemba 25 mwaka 2014. REUTERS/Adrees Latif
Matangazo ya kibiashara

Kufwatia ripoti hiyo, Meya wa mji wa Ferguson, katika jimbo la Missouri, James Knowles, amesema hatua kadhaa zimechukuliwa dhidi ya polisi wa mjini humo kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi, na kuthibitisha kuwa mwajiriwa mmoja toka Idara ya Polisi amefukuzwa kazi huku wengine wawili wamepewa kwenda likizo baada ya kushutumiwa kutuma barua pepe yenye ujumbe wa kibaguzi.

Knowles amesema Idara ya sheria itaongeza idadi ya maafisa wasio wazungu na kujikita katika mafunzo.

Hayo yakijiri kesi ya Djokhar Tsarnaev imefunguliwa katika mji wa Boston, ikiwa ni pamoja na hotuba ya ufunguzi wa mashitaka na utetezi, pamoja na ushadidi wa waathiriwa kadhaa wa shambulio liliotokea Aprili mwaka 2013.
Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu watatu, ikiwa ni pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 8 na watu 263 kujeruhiwa wakati wa mbio za Marathon.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Jean-Louis Pourtet, mwanasheria wa Djokhar Tsarnaev hakukanusha kuwa mteja wake alishiriki katika mashambulizi hayo, hata kama amekiri kuwa hana hatia kwa makosa 30 anayotuhumiwa, ikiwa ni pamoja na kosa la kutumia silaha ya maangamizi na kusababisha kifo