MAREKANI-VENEZUELA-MVUTANo-DIPLOMASIA

Mvutano wa kidiplomasia waibuka kati ya Marekani na Venezuela

Marekani na Venezuela zimefikia katika hatua ya vita vya kidiplomasia, baada ya serikali ya Caracas kuamuru tangu mwanzoni mwa mwezi Machi kwa raia wa Marekani kuwa na viza kwa kuingia Venezuela.

Kibonzo kinachoashiria kupigwa vita kwa Marekani katika mji wa Caracas, Machi 9 mwaka 2015.
Kibonzo kinachoashiria kupigwa vita kwa Marekani katika mji wa Caracas, Machi 9 mwaka 2015. REUTERS/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii, Marekani imewachukulia vikwazo viongozi wengi wa Venezuela, ambao inawatuhumu kukiuka haki za binadamu.

Mvutano huo kati ya nchi hizi mbili umeendelea kukua, wakati ambapo nchi ya Venezuela ikishuhudia mdororo wa kiuchumi, huku upinzani kwa rais Nicolas Maduro ukiendelea kukabiliwa na vitisho ili kujaribu kuunyamanzisha.

Tangazo la vikwazo kwa viongozi wa Venezuela limetolewa na rais wa Marekani, Barack Obama.

“ Mimi, Barack Obama, naona kuwa hali ya Venezuela ni tishio kwa usalama wa taifa na sera za nje za Marekani”, amesema rais Obama. Kila nchi kati ya Venezuela na Marekani , imechukua msimamo.

Rais wa Marekani ametia saini kwenye sheria ya kirais inayozidisha vikwazo dhidi ya maafisa waandamizi 7 wakiwemo wale wa zamani, ambao wote ni maafisa wa ngazi ya juu au waliwahi kuhudumu katika polisi, vyombo vya sheria na jeshi la Venezuela.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, maafisa hao waandamizi walishiriki katika kuawakandamiza waandamanaji waliokua wakiandamana dhidi ya serikali. Maandamano ambayo yaligharimu maisa ya watu 43 mwaka 2014.

Maafisa hao watanyimwa viza na mali zao kuzuiliwa. Ikulu ya White House imeelezea wasiwasi wake kwa namna wapinzani wanavyonyanyaswa na viongozi wa Caracas.