MAREKANI-FERGUSON-MAANDAMANO-Usalama

Ferguson, hasira yapanda siku baada ya siku

Maafisa wawili wa polisi walikuwa wamewekwa wakipiga doria mbele ya ofisi ya polisi ya Ferguson walipojeruhiwa kwa  risasi Jumatano jioni.
Maafisa wawili wa polisi walikuwa wamewekwa wakipiga doria mbele ya ofisi ya polisi ya Ferguson walipojeruhiwa kwa risasi Jumatano jioni. REUTERS/Lawrence Bryant/St. Louis American

Waziri wa sheria wa Marekani, Eric Holder, amelani machafuko yanayoendelea katika mji wa Ferguson.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi walijeruhiwa kwa risasi Alhamisi jioni wiki hii. Mji huo mdogo wa jimbo la Missouri umeendelea kushuhudia machafuko tangu mwezi Agosti mwaka jana na baada ya kifo cha Michael Brown, kijana mweusi aliyeuawa na askari polisi.

Ripoti ya serikali ya jimbo la Missouri inaonesha kuwa kumekua na ubaguzi wa rangi toka katika ngazi za juu za viongozi wa maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Kwa sasa kumekua kukishuhudiwa kufutwa kazi na kujiuzulu kwa siri kwa viongozi mbalimbali, lakini hali hiyo haizui waandamanaji kuingia mitaani.

Polisi katika mji wa Ferguson wanatambua kuwa risasi ziliyowajeruhi wenzao zilifyatuliwa na watu waliokuwa walijiweka kando, wakati wa maandamano.

Kwa upande wao, familia ya Michael Brown na viongozi wa vuguvugu la watu wenye hasira dhidi ya unyanyasaji wa polisi hawaungi mkono hali hii, lakini wamesema vitendo vya kuwafyatulia risasi askari polisi vimeendelea kukua kutokana na dhuluma ambayo wameendelea kufanyiwa kwa kipindi cha miaka kadhaa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Anne-Marie Capomaccio, waziri Eric Holder ameanza kushughulikia ripoti ya serikali juu ya ukiukwaji wa polisi dhidi ya jumuiya ya watu weusi katika mji wa Ferguson. Waziri Eric Holder ana imani kwamba juhudi zake hazitadhoofishwa na chokochoko ya aina hii.

" Ninalaani mashambulizi haya ya kinyama. Vitendo hivi vya kinyama na ujinga vimetekelezwa bila shaka kwa lengo la kudhoofisha mafanikio ambayo tumefikia, na nafikiri hali hiyo haitatokea", amesema Waziri Holder.