BRAZIL-MAANDAMANO-USALAMA

Brazili : takribani watu milioni moja na nusu waandamana

Raia milioni 1.5wa Brazili wakiandamana mjini Sao Palo, wakikemea kashfa ya Petrobras na kupinga siasa ya rais Dilma Rousseff.
Raia milioni 1.5wa Brazili wakiandamana mjini Sao Palo, wakikemea kashfa ya Petrobras na kupinga siasa ya rais Dilma Rousseff. REUTERS/Paulo Whitaker

Takribani watu milioni moja na nusu wa Brazili wameingia mitaani Jumapili Machi 15 wakiandamana dhidi ya rais wa taifa hilo ambaye ni kutoka mrengo wa kushoto, Dilma Rousseff.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yamefanyika katika miji 74 ikiwa ni pamoja na Sao Paulo, mji mkuu wa kiuchumi ambapo watu 580,000 wameandamana kulingana na mahesabu ya jeshi la polisi.

Waandamanaji wamekua wakimtaka Dilma Rousseff ajiuzulu. Dilma Rousseff alichaguliwa, baada ya kuponea kushindwa, mwaka 2014 kwa muhula wa pili wa miaka minne.

Maandamano kama haya ya kumpinga rais Dilma Rousseff yalifanyika mwezi Juni mwaka 2013, wakati ambapo wananchi walikua wakipiga kelele kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha licha ya Dilma Rousseff kuahidi kufanya mabadiliko ili kuhakikisha anatii kiu ya wananchi wake.

Wakati huo mamia kwa maelfu ya waandamanaji walijitokeza kwenye mitaa ya Rio De Janeiro na Sao Paoul na kufunga barabara wakionesha kuchukizwa na ahadi ambazo zilitolewa na rais Rousseff ya kuhakikisha anaboresha huduma za usafiri, elimu na afya.