MAREKANI-ISRAELI-SIASA-USALAMA_DIPLOMASIA

Marekani yalaani matamshi ya Netanyahu

Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye utawala wake umelani matamshi ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin netanyahu ya kuapa kutokubali kuundwa kwa taifa la Palestina.
Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye utawala wake umelani matamshi ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin netanyahu ya kuapa kutokubali kuundwa kwa taifa la Palestina. REUTERS/Mandel Ngan/Pool

Marekani imekosoa matamshi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu , kuwa hatakubali kuundwa kwa taifa la Palestina kama njia mojawapo ya kumaliza mzozo kati ya Israeli na Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Marekani inasema matamshi ya Netanyahu yanarudisha nyuma uwezekano wa kuwepo kwa mazungumzo ya amani, baada ya chama cha Netanyahu cha Likud kushinda uchaguzi wa wabunge Jumatano wiki hii.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliapa kuwa hakutakua na taifa huru la Palestina kama atakua bado madarakani.

Msemaji wa rais Barrack Obama, Josh Earnest amesisitiza kuwa Washington inaunga mkono uundwaji wa taifa la Palestina kama njia ya kupata amani ya Mashariki ya Kati.

Netanyahu, anakuwa Waziri mkuu wa Israeli aliyehudumu kwa muda mrefu wa mihula minne.