Barack Obama awasihi raia wa Iran
Imechapishwa:
Rais wa Marekani Barrack Obama amewaambia wananchi wa Iran kuwa kufikiwa kwa mkataba kuhusu mradi wake wa Nyuklia, utasaidia kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Obama ameutoa ujumbe huo kwa wananchi wa Iran wakati wakiadhimisha mwaka mpya na kusisitiza kuwa, viongozi wa Iran wana nafasi ya kuamua mustakabili wao na Jumuiya ya Kimataifa hasa.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anaongoza mazungumzo kuhusu mradi huo wa nyuklia nchini Uswisi na makubaliano yanatarajiwa kuifikiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu lakini wanadilomasia wanasema bado kuna kazi kubwa ya kufanya.
Rais Barack Obama amesema mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran yamepiga hatua lakini ameonya kuwa kuna watu wanaopinga mazungumzo juu ya mpango huo kwa nchi zote mbili yaani Marekani na Iran.
Obama amesema raia wa Iran watakabiliwa na matatizo zaidi kwa kutengwa kimataifa iwapo viongozi wao watachukua uamuzi usio sahihi.