Singapore-maombolezo

viongozi wa dunia watuma Salam za rambirambi kwa viongozi wa Singapore

Viongozi mbalimbali wa Dunia wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa viongozi wa nchi ya Singapore kufuatia kifo cha waziri mkuu wake wa kwanza, Lee Kuan Yu aliyefariki akiwa na umri wa miaka 91.

wananchi wa singapore wakitowa shahada za maua kufuatia kifo cha Lee Kuan Yew
wananchi wa singapore wakitowa shahada za maua kufuatia kifo cha Lee Kuan Yew Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Singapore ni rais wa Marekani Barack Obama ambaye amemuelezea, Lee kama mtu aliyekuwa na maono na mpigania demokrasia si tu kwa nchi ya Singapore bali kwa eneo zima bara la Asia.

Mtoto wa Lee, ambaye pia ni waziri mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong amesema wamepoteza kiongozi shupavu atakayekumbukwa kwa mchango wake kwa taifa lao ambalo sasa ni mfano bora wa demokrasia na uchumi ulioimara kutokana na utawala wake, ambapo amewataka wananchi kumuenzi vyema baba yake.

Lee alikuwa waziri mkuu toka mwaka 1959 wakati ambapo wakoloni wa kiingereza waliitangaza nchi hiyo kama taifa huru mpaka mwaka 1990 ambapo aliiongoza Singapore kupata uhuru kamili mwaka 1965 baada ya muungano wao na Malaysia.