MAREKANI-SIASA

Rand Paul atangaza kugombea uchaguzi wa urais Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye hatagombea katika uchaguzi wa urais ujao, baada ya kukmilisha mihula yake miwili akiwa madarakani.
Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye hatagombea katika uchaguzi wa urais ujao, baada ya kukmilisha mihula yake miwili akiwa madarakani. REUTERS/Kevin Lamarque

Seneta mwenye umaarufu kutoka Kentucky wa chama cha Republican nchini Marekani Rand Paul, amekuwa mwanasiasa wa kwanza kujitokeza na kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Rand Paul ameyasema hayo kupitia akaunti yake ya twitter na pia tovuti yake huku akizindua kampeni zake anazoziendesha kupitia mitandao ya kijamii kubainisha kuwa anataka kuirejesha nchi hiyo katika kanuni za uhuru.

Rand Paul ameungana na seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz, katika harakati hizo ambazo zimevuta hisia za nusu ya wagombea wakubwa wa chama cha Republican, na hii ni pamoja na gavana wa zamani wa jimbo la Florida Jeb Bush, gavana wa Wesconsin Scott Walker,ambaye bado hajatoa tamko lake rasmi .

Hayo yakijiri mkuu wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA, John Brennan amewatuhumu wanasiasa pamoja na wadau wengine wa kimataifa kudhihirishwa kutofurahishwa na makubaliano ya hivi karibuni kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Bwana Brennan ameuhakikishia ulimwengu kwamba hakuna la kuhofia kuhusu uwezekano wa taifa la Iran kuendeleza mpango wake huo wa kutengeneza silaha za maangamizi makubwa kisiri.

Akizungumza na wanafunzi katika chuo kikuu cha Harvard, John Brennan amesema wako makini kuifwatilia Teheran ambayo imepewa muda maalum kusitisha urutubishwaji wa uranium.