MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Obama na Castro wapeana mkono

Viongozi kutoka nchi 35 za Amerika wanakutana mjini Panama katika mkutano wa kilele ambao ni wa kihistoria unaofanyika kila mwaka.

Raul Castro na Barack Obama katika ufunguxzi wa mkutano wa kilele wa viongozi kutoka nchi za Amerika unaofanyika Panama, Aprili 10 mwaka 2015.
Raul Castro na Barack Obama katika ufunguxzi wa mkutano wa kilele wa viongozi kutoka nchi za Amerika unaofanyika Panama, Aprili 10 mwaka 2015. REUTERS/Panama Presidency
Matangazo ya kibiashara

Cuba ikiwa ni kwa mara ya kwanza inawakilishwa katika mkutano huo, rais wa nchi hiyo Raul Castro amepeana mkono na rais wa Marekani Barack Obama kabla ya kuchangia chakula cha jioni cha ufunguzi wa mkutano. Wawili hao wanatazamiwa kukutana rasmi leo Jumamosi.

Itakua ni mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya marais wa Marekani na Cuba tangu mwaka 1959.

Barack Obama, katika hotuba yake kwa asasi za kiraia, alitamka maneno kuhusu uhusiano kati ya Washington na nchi za Amerika ya Kusini.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Anne-Marie Capomaccio, mkutano huu wa Amerika ni dhahiri mkutano unaoleta sura mpya kati ya nchi za bara hilo. Barack Obama ameshangaza wengi katika mkutano huo akielezea mwenendo wa Marekani kuingilia kati masuala ya nchi za Amerika ya Kusini, na mahusiano wakati mwingine mabaya kati ya Washington na baadhi ya serikali.

" Katika enzi ambapo ajenda yetu ya kisiasa katika ulimwengu iliyokua ikielezwa kuwa Marekani ilikua ikiingilia kati masuala ya nchi fulani bila hata hivyo kuchukuliwa vikwazo, enzi hizo zimekwisha", amesema rais wa Marekani.

Ukurasa mpya unaoelezwa pia katika mkutano huo, ni kufufuka kwa uhusiano kati ya marais wa Cuba na Marekani. Marais hao wawili wamepeana mkono kabla ya mkutano huo kuanza Ijumaa jioni wiki hii. Barack Obama na raul Castro wamechangia pia chakula cha jioni kwenye meza moja wakiandamana na mwakilishi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis. Papa Francis ndie aliyefanya jitihada za kukutanisha viongozi wa mataifa hayo mawili kwa lengo la kufufua uhusiano kati ya Havana na Washington.