MAREKANI-CLINTON-UCHAGUZI=SIASA

Hillary Clinton atangaza kuwania urais mwaka 2016

Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton amezindua rasmi kampeni ya kusaka tiketi ya chama chake cha Democratic kuwania urais mwaka ujao.

Hillary Clinton, hapa akiwa katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Desemba3 mwaka 2014, kwa sasa ametangaza rasmi kuingia katika kinyang'anyiro cha urais.
Hillary Clinton, hapa akiwa katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Desemba3 mwaka 2014, kwa sasa ametangaza rasmi kuingia katika kinyang'anyiro cha urais. REUTERS/Kevin Lamarque/Files
Matangazo ya kibiashara

Bi Clinton amezindua kampeni zake kupitia mitandao ya kijamii na amewaambia Wamarekani kuwa anataka kuwa bingwa wao.

Bi Clinton mwenye umri wa miaka 67 mwaka 2008 alijaribu kupata tiketi ya chama chake cha Democratic lakini akashindwa na rais wa sasa Barack Obama.

Waangalizi wa mambo wanasema wakati huu Bi Clinton ana nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya chama chake wakati wa uchaguzi wa urais mwezi Novemba mwaka ujao wa 2016.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa hasa kutokana na sera zake hususan katika sekta ya teknolojia.

Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amempongeza Hillary clinton na kumtakia ushindi katika kinyang'anyiro hicho, huku akiwa na matumaini kuwa ataibuka mshindi katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2016.