CUBA-MAREKANI-DIPLOMASIA

Cuba yakaribisha hatua ya Marekani

Bendera za marekani zikipambwa kwenye teksi na kwenye baiskeli za kukodiwa jijini Havana, Cuba, Januari 26 mwaka 2015.
Bendera za marekani zikipambwa kwenye teksi na kwenye baiskeli za kukodiwa jijini Havana, Cuba, Januari 26 mwaka 2015. AFP PHOTO/Yamil LAGE

Nchi ya Cuba imepongeza hatua ya Marekani kuiondoa kwenye orodha ya nchi ziinazofadhili ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Cuba imesema hatua hiyo ya Marekani itaimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili lakini ikasisitiza kuwa haikustahili kuwa katika orodha hiyo ya Marekani.

Hatua hii imekuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya viongozi wa nchi hizi mbili na baada ya rais Barrack Obama na Raul Castro kukutana juma lililopita.
Pamoja na Cuba, Marekani pia imeiorodhesha nchi Syria, Iran na Sudan kama nchi zinazofadhili ugaidi duniani.

Rais Obama amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika kuwa kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, serikali ya Cuba haijatoa msaada wowote kwa kundi liolote la kigaidi duniani.

Marekani iliiorodhesha Cuba mwaka 1982 kwa tuhma za kuchochea mapinduzi ya nguvu na kuunga mkono ugaidi, na imekuwa ikiamini kuwa nchi hiyo inatumiwa kuwapa hifadhi makundi ya waasi kama FARC kutoka Colombia.

Haaa hivyo uamuzi huo umeshtumiwa na wabunge wa Republican na hasa Senata Marco Rubio aliyetangaza nia ya kuwania urais, na kusema Cuba bado inasalia nchi inayounga mkono ugaidi.