MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Marekani yaiondoa Cuba kwenye orodha ya wafadhili wa ugaidi

Marais wa Cuba na Marekani, Raul Castro na Barack Obama wakipeana mkona, ikiwa ni ishara ya kihistoria, wakati wa mkutano wa kilele wa nchi za Amerika, Jumamosi Aprili 11 mwaka 2015.
Marais wa Cuba na Marekani, Raul Castro na Barack Obama wakipeana mkona, ikiwa ni ishara ya kihistoria, wakati wa mkutano wa kilele wa nchi za Amerika, Jumamosi Aprili 11 mwaka 2015. REUTERS/Jonathan Ernst

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya White House, Rais Barack Obama alionya Jumanne Aprili 14 Bunge la Congress kwamba alikua na nia ya kuondoa Cuba kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugadi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Iwapo Bunge la Congress litaidhinisha uamuzi huu, moja ya vikwazo vikuu viliyoleta uhasama katika mahusiano kati ya nchi hizo mbili kitakua kimeondolewa.

Katika ripoti iliyowasilishwa kwa Bunge la Congress, rais wa Marekani amesema kwamba "serikali ya Cuba haikutoa msaada wowote kwa ugaidi wa kimataifa katika kipindi cha miezi sita. "

Kulingana na taratibu za sasa, Wizara ya mambo ya ndani itawasilisha mapendekezo yake kwa Bunge la Congress ya kuiondoa Cuba kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani.

Wabunge wanazo siku arobaini na tano kwa kukubali au kupinga mapendekezo hayo. Iwapo Wabunge watapinga kupitisha uamzi huo, Obama anaweza kutumia kura yake ya turufu. Uamuzi huo unapaswa kuungwa mkono na idadi kubwa ya viongozi waliochaguliwa. Lakini bila shaka, baadhi wanapinga, hata miongoni mwa viongozi kutoka chama cha Democrat. Kati yao, Seneta Robert Menendez, mwenye asili ya Cuba. Kwa upande wa chama cha Republican, Marco Rubio, pia mwenye asili ya Cuba amepinga uamzi wa Obama, akitaja kuwa uamzi huo " haufai ". Rubio amesema kuwa Cuba bao inaendelea kuunga mkono ugaidi.

Lakini John Kerry amesema : " Mazingira yamebadilika tangu 1982." Kama Cuba iliondolewa kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani, inaweza kuwa na matumaini ya kufunguliwa kwa ubalozi wake nchini Marekani pamoja na kuruhusiwa kuingia katika mfumo wa benki za Marekani. Cuba iliwekwa kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani tangu mwaka 1982, ikiwa kwenye orodha moja na Syria, Sudan na Iran. hata hivyo uhasama wa kidipolomasia kati ya Washington na havana ulikuepo tangu mwaka 1961.

Cuba imekaribisha uamzi huo wa Obama wa kuindoa kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani, huku ikibaini kwa haijawahi kufadhili ugaidi.