USA-MOTO-JAMII-USALAMA

USA: moto wateketeza misitu California, familia 300 zahamishwa

Maeneo ya kusini mwa California, Marekaniani yanakumbwa na ukame pamoja na majanga ya moto ambao umeteketeza misitu na mashamba.
Maeneo ya kusini mwa California, Marekaniani yanakumbwa na ukame pamoja na majanga ya moto ambao umeteketeza misitu na mashamba. REUTERS/Gene Blevins

Moto mkali unaendelea kuteketeza misitu kusini mwa California nchini marekani tangu Jumamosi Aprili 18. Zaidi ya familia 300 waliokolewa katika hekta 125.

Matangazo ya kibiashara

Moto huu mkubwa ni nadra katika msimu huu, na viongozi wanabaini kuwa ukame unaoathiri kanda hiyo umesababisha hali hiyo kuongezeka.

Jumapili Aprili 19, maafisa wa kuzima moto walijielekeza eneo hilo, lakini wameshindwa kudhibiti moto huo, ambao umeendelea kuongezeka kwa kiwango kikubwa na kusababisha kitisho kikubwa kwa familia za watu 300 na kuteketeza mashamba kusini mwa California.

Helikopta na ndege zinazokabiliana na majanga ya moto zimekua zikizima moto, wakati ambapo moto huo umeendelea kushika kasi kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa. Viongozi wametenga maeneo ya malazi ya dharura, na operesheni ya kuwaokoa wanyamapori inaendelea.

Ukame isiyokuwa wa kawaida unaoathiri kanda hiiyo ni ni sababu moja wapo, inayoathiri udongo na mimea ambavyo vinakosa maji na kusababisha moto kuendelea kushika kasi, ambapo mashahidi wanaweza kuona kwa kilomota kadhaa wakiwa mbali.

Kwa mwaka wa nne mfululizo, Jimbo hilo la california unakabiliwa na uhaba wa maji, meza maji ni mdogo. Wakaazi milioni 40 wa California wametakiwa kufanya akiba kwa misingi ya hiari. Na kwa sasa wamelazimishwa kupunguza matumizi ya maji kwa asilimia 25 la sivyo wametakiwa kutozwa faini.