CHILE-VOLCANO-USALAMA

Volcano yalipuka Chile

Milipuko mikali miwili ambayo haikua inatarajiwa imeshangaza wakaazi wa jimbo la Los Lagos, kusini mwa Chile. Volcano hiyo aina ya Calbuco ilikua haifanyi kazi tangu nusu karne.

Eneo lililo karibu na volcano Calbuco kusini mwa Chile, liliwekwa katika tahadhari nyekundu baada ya mlipuko wa volkano, Aprili 22.
Eneo lililo karibu na volcano Calbuco kusini mwa Chile, liliwekwa katika tahadhari nyekundu baada ya mlipuko wa volkano, Aprili 22. REUTERS/Rafael Arenas
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa kwanza wa Calbuco uliyosikika karibu na mji wa Puerto Montt, umewashangaza wengi. Mlipuko wa pili ulitokea saa chache baadaye, Alhamisi asubuhi Aprili 23. Kwa sasa, kijana mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa kilomita moja kutoka eneo la volcano hajulikani alipo. Ilani nyekundu imetolewa katika jimbo hilo, huku zaidi ya wakaazi 4000 wa eneo lililo karibu na Volcano wamehamishwa na kupelekwa kwenye umbali wa kilomita 20 na eneo la Volcano hiyo.

Rais wa Chile Michelle Bachelet, ambaye anasubiriwa kwenye eneo hilo Alhamisi wiki hii, alifanya mkutano na waandishi wa habari Jumatano jioni wiki hii.

" Idara ya kitaifa ya masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na madini ilitutaarifu kuhusu uwezekano wa kulipuka kwa volcano hiyo ", amesema rais Michelle Bachelet.

Chile inachukuliwa kama nchi ya pili yenye volcano nyingi duniani baada ya Indonesia. Chile ina takriban volcano 2000, huku 500 zikiwa bado hai. Mwezi Machi Volcano ya Villarrica ililipuka, na kulazimisha zaidi ya watu 3,500 kuyahama makaazi yao.

Picha za televisheni zilionyesha wingu zito na majivu vikipanda hewani umbali kilomita kadhaa angani katika jimbo la Los Lagos kusini mwa Chile.