MAREKANI-BALTIMORE-MAUAJI-USALAMA

Barack Obama aionya polisi Baltimore

Jumanne jioni Aprili 28 mwaka wanajeshi na askari polisi wametumwa kupiga doria katika mji wa Baltimore.
Jumanne jioni Aprili 28 mwaka wanajeshi na askari polisi wametumwa kupiga doria katika mji wa Baltimore. Mark Makela/Getty Images/AFP

Maelfu ya wanajeshi na askari polisi wametumwa Jumanne jioni wiki hii katika mji wa Baltimore, baada ya utawala katika mji huo kutangaza hali ya hatari, na kuwataka wakaazi mji huo kutotoka nje usiku.

Matangazo ya kibiashara

Rais Barack Obama wa Marekani ameionya polisi Mjini Baltimore katika jimbo la Maryland kuchukua tahadhari , kufwatia machafuko na moto uliowashwa kila maeneo, siku moja baada ya kutangazwa amri ya kutotoka nje mjini humo.

Wananchi wa Baltimore wamezusha ghasia wakati wa mazishi ya kijana Mmarekani mweusi Freddie Gray aliyefariki baada ya kupata maumivu katika uti wa mgongo wakati alipokua akishikiliwa na polisi.

Machafuko hayo, ambayo yalishuhudia waporaji walivunja maduka, maduka ya dawa na majengo yenye maduka mengi na kupambana na polisi.