MAREKANI-BALTIMORE-MAANDAMANO

Maandamano dhidi ya unyanyasaji ya watu weusi Marekani

Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikubwa nchini Marekani kushinikiza polisi kuacha kuwanyanyasa watu wenye asili ya Afrika.

Maandamano Baltimore Jumamosi Aprili 25 ya kupinga dhidi ya kifo cha kijana mweusi, raia wa Marekani.
Maandamano Baltimore Jumamosi Aprili 25 ya kupinga dhidi ya kifo cha kijana mweusi, raia wa Marekani. REUTERS/Sait Serkan Gurbuz
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yamefanyika baada ya kijna mmoja mwenye asili ya Kiafrika kuuawa alipokuwa anazuiliwa na polisi katika mji wa Baltimore katika jimbo la Maryland juma lililopita.

Katika mji wa Baltimore waandamanaji waliokuwa na hasira walihakikisha kuwa shughuli zote zinasimama wakati wa maandamano hayo.

Miji ambayo imeshuhudia maandamano hayo mbali na Baltimore ni pamoja na New York, Boston na jiji kuu la Washington DC.

Maandamano ya leo yamekuwa ya amani katika miji yote.
Siku mbili zilizopita katika mji wa Baltimore polisi walikabiliana na waandamanaji ambao waliamua kupora na kuvamia watu baada ya kuawa kwa kijana huyo mweusi.