FIFA-BLATTER-KUJIUZULU-SHERIA

Fifa: Blatter ajiuzulu kwenye wadhifa wake

Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17.
Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17. REUTERS/Arnd Wiegmann

Sepp Blatter, raia wa Uswisi, ambaye alichaguliwa kwa muhula wa tano Mei 29 kuliongoza Shirikisho la Soka Duniani Fifa, ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne Mei 2 katika mji wa Zurich kwamba amejiuzulu kwenye wadhifa wake.

Matangazo ya kibiashara

Uamzi huu unakuja kufuatia kashfa ya rushwa inayolikabili Shirikisho la Soka Dunia Fifa tangu Mei 27.

Akiwa ni mwenyekiti wa Fifa tangu mwaka 1998, Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu Jumanne wiki hii katika mji wa Zurich, siku tano baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa tano kama mwenyekiti wa Shirikisho hilo la kandanda Duniani.

“ Nataka kuitisha mkutano wa dharura na kukabidhi muhula wangu kwa yoyote yule atakayeshinda katika kinyanga'nyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Fifa”, amesema Blatter.

Sepp Blatter na timu yake wanatuhumiwa kutoa kiholela masoko ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi na Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

“ Hata kama nilichaguliwa, sikupata uungwaji mkono wa pande zote ”, amesema Blatter katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Fifa.

Sepp Blatter, mwenye umri wa miaka 79, amekua akishikilia wadhifa huo tangu mwaka 1998. Mswisi huyo amebaini kwamba ataitisha mkutano wa dharura kati ya mwezi Desemba mwaka 2015 na Machi mwaka 2016.

“ Ntaendelea kushikilia wadhifa wangu kwa muda wa miezi kadhaa, kabla ya kumkabidhi mwenyekiti mpya atakaye kuwa amechaguliwa", ameongeza Joseph Sepp Blatter.

Ni uamzi mzuri, kwa mujibu wa Michel Platini

Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (Uefa), Michel Platini, amekaribisha uamzi huo wa Sepp Blatter. Lakini baadhi ya marais wa mashirikisho ya Soka kutoka mataifa ya Afrika wameshtushwa na uamzi huo, hasa Constant Omari, rais wa shirikisho la Soka la Congo, ambaye amemsifu Sepp Blatter kuwa ni mtu jasiri na mwenye uamzi.