MAREKANI-CHARLESTON-MAUAJI-USALAMA

Waumini wafurika katika ibada ya Charleston

Dylann Roof Dylann akichoma moto bendera ya Marekani.
Dylann Roof Dylann akichoma moto bendera ya Marekani. Reuters

Mamia ya watu walifurika katika Kanisa la watu weusi la Kimethodisti mjini Charleston nchini Marekani jana Jumapili kuwakumba watu tisa waliuawa baada ya kupigwa risasi na kijana mzungu juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Waumini waliongia ndani ya kanisa hilo walichunguzwa mlangoni na maafisa wa usalama waliofika kuhakikisha kuwa kuna usalama baada ya tukio hilo.

Watu wengi kutoka maeneo ya jirani walikusanyika nje ya kanisa hilo kushiriki misa hiyo ya maombolezo. Ilikuwa ni ibada ya kwanza kanisani hapo tangu siku ya Jumatano iliyopita kulipofanyika shambulio hilo.

Nje ya Kanisa hilo pia kulikuwa na wazungu waliokuja kuungana na Wamarekani hao weusi kuwakumbusha waliopoteza maisha.Mmoja ya waliouawa alikuwa ni mchungaji Clementa Pinckney.

Kijana aliyetekeleza mauaji hayo Dylann Roof amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.