MAREKANI-URUSI-UKRAINE-IS

Obama na Putin wazungumzia suala la Ukraine na IS

Barack Obama na Vladimir Putin, mwaka 2012, Mexico.
Barack Obama na Vladimir Putin, mwaka 2012, Mexico. AFP PHOTO/Jewel Samad

Rais wa Marekani Barrack Obama amezungumza na mwezake wa Urusi Vladimir Putin kuhusu usalama Mashariki mwa Ukraine, mashambulizi ya Islamic State nchini Iraq na Syria pamoja na suala la Nyuklia la Iran.

Matangazo ya kibiashara

Mzozo wa Mashariki mwa Ukraine umesababisha mvutano kati ya Marekani na Urusi, na mapema juma hili Marekani ilitanagza kutuma silaha nzito Mashariki mwa Ulaya.

Rais Obama amemwambia rais Putin kuondoa wanajeshi wake katia mji wa Minsk kama ilivyokubaliwa wakati wa mazungumzo ya amani.

Wakati huo huo Mahakama ya rufaa nchini Marekani imepitisha sheria ya bima ya afya ya Obamacare.

Kati ya majaji 9, sita waliunga mkono huku wengine watatu wakipinga sheria hiyo ambayo rais Obama anasema itawasaidia Wamarekani wenye maisha ya kati kupata huduma za matibabu.

Wanasiasa wa upinzani wa chama cha Republican wanapinga sheria hiyo inayolnega kuwatoza kodi kubwa matajiri nchini humo kuchangia katika mfuko wa bima hiyo ya afya.