ISRAEL-MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USHIRIKIANO

Israel: majenerali wa zamani waunga mkono makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran

Majenerali wa zamani wa Israel na wakuu wa Idara ya Ujasusi na vyombo vya usalama wametoa wito kwa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu kukubali mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, ambao anaendelea kupiga vita akijaribu kuhamasisha Bunge la Marekani.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ana nia ya kujaribu kuzuia Bunge la Marekani kupitisha mkataba wa Vienna.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ana nia ya kujaribu kuzuia Bunge la Marekani kupitisha mkataba wa Vienna. REUTERS/Abir Sultan/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Jerusalem, Michel Paul, orodha ya waliosaini waraka huo ni ndefu. Na idadi kubwa ya maafisa wa zamani wa usalama nchini Israeli, kama vile Ami Ayalon na Karmi Gillon, wakuu wawili wa zamani wa Shin Bet, Idara ya usalama wa ndani, Amiram Levine, aliyekuwa namba mbili wa Mossad, kitengo cha Idara ya Ujasusi , mkurugenzi wa zamani wa Tume ya nishati ya atomiki pamoja na zaidi ya majenerali wa zamani kumi na maafisa waandamizi katika vyombo vya usalama na ulinzi.

Ujumbe huu uko wazi: maafisa hao wametoa wito kwa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu kukubali mkataba wa Vienna mkataba. Waraka huo, unabaini, mkataba huo tayari umefikiwa. Na ndiyo maana wametoa mapendekezo kwa serikali ya Israel kupitisha sera yenye uwezo wa kurejesha imani na ushirikiano wa kidiplomasia na usalama pamoja na Marekani.

Maafisa hao wameongeza kwamba uhusiano mzuri na Washington unahitajika kwa kukabiliana na changamoto nyingi ambazo zinatokana na mkataba huo. Binjamin Netanyahu, kwa upande wake, bado ana nia ya kujaribu kuzuia ili makubaliano hayo yasiwezi kupitishwa na Bunge la Marekani na bado ameendelea msimamo wake wa kupambana na rais Barack Obama.