MAREKANI-CHINA-URUSI-DIPLOMASIA

Kerry azituhumiwa China na Urusi kusoma barua pepe zake

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, Jumanne wiki hii amezituhumu nchi za China na Urusi kusoma kwa "uwezekano mkubwa" barua pepe zake na kuonya kuwa suala la udukuzi wa mitandaoni litajadiliwa na Barack Obama mwezi Septemba atakapompokea mwenzake wa China, Xi Jinping.

John Kerry apiga picha milima ya Uswisi wakati akisafiri katika helikopta kati ya Zurich na Davos, Januari 25 mwaka 2014.
John Kerry apiga picha milima ya Uswisi wakati akisafiri katika helikopta kati ya Zurich na Davos, Januari 25 mwaka 2014. AFP/POOL/AFP/Archives -
Matangazo ya kibiashara

" Jibu ni kwamba huu ni uwezekano mkubwa. Wala sio kando ya suala la uwezekano na tunajua Cina na Urusi walishambuliwa kiwango cha maslahi ya Marekani katika siku za za hivi karibuni ", Kerry amesema katika mahojiano na televisheni CBS.

John Kerry alikuwa akijibu mtangazaji wa televisheni hiyo ambaye alimuuliza iwapo "anadhani kwamba China au Urusi zimekua zikisoma barua pepe zake".

" Kwa bahati mbaya, tunaishi katika ulimwengu ambapo baadhi ya nchi, ikiwa ni pamoja na China na Urusi walihusika katika mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani, dhidi ya serikali ya Marekani ", John Kerry ameongeza.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amekumbusa kwamba Marekani " hivi karibuni ilizungumzia suala hili, kwa umakini, katika mazungumzo yetu na viongozi wa China ".

" Suala hili linatakua katika ajenda yamazungumzo kati ya rais Obama na rais Xi watakapokutana mwezi Septemba katika Ikulu ya Marekani kwa ziara ya kikazi ", amesema Kerry.