Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Maridhiano kati ya Cuba na USA: mashaka na matumaini ya Wacuba

Njia panda ya Havana, karibu na kituo cha historique.
Njia panda ya Havana, karibu na kituo cha historique. RFI/Véronique Gaymard
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, atakuwa nchini Cuba leo Ijumaa kwa ziara ya kihistoria ambayo inatazamiwa kufuafua rasmi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Washington na Havana.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, ubalozi wa Marekani ulifunguliwa rasmi mjini Havana tarehe 20 Julai, lakini ziara ya John Kerry inaashiria mambo mengi. Kupandishwa kwa bendera mbele ya ubalozi na sherehe kubwa itakayofuata vitaashiria uhusiano huu wa kihistoria.

Maridhiano haya yanawatia hofu wapinzani wengi wa Cuba lakini watu wengi wana matumaini na maridhiano hayo.

Wakati wa ziara yake nchini Cuba, John Kerry amepanga kukutana na wapinzani. Lakini mkutano huo utakua wa faragha, wanahabari hawataruhusuwa kuhudhuria mkutano huoutakaofanyika katika ubalozi wa Marekani. Jambo ambalo llinaonekana kuwatia hofu baadhi ya upinzani nchini Cuba.

Jumapili iliyopita wapinzani wengi nchini Cuba waliingia mitaani mjini Havana wakimpinga rais wa Marekani. Wapinzani hao walisema kuwa wana wasiwasi juu ya kumpoteza mshirika wao mkuu, ambaye ni Marekani, katika mapambano yao dhidi ya serikali iliopo madarakani.Katika maandamano hayo watu 90 walikamatwa.

Hofu hiyo ya kumpoteza mshirika imara haiwahusu wapinzani wote nchini Cuba kwa mujibu wa Sebastian Arcos, mfungwa wa zamani wa kisiasa na mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Tathmini ya Chuo kikuu cha Florida.

" Kuna baadhi ya wapinzani ambao wanaamini kwamba pamoja na mabadiliko, yaliofanywa na upande mmoja tena bila masharti, wamepoteza nafasi ya kuweka shinikizo kwa serikali ya Cuba, kwa hiyo, mabadiliko haya yamefuta ushirikiano wa Marekani kwa wapinzani, ambapo upinzani ulichukuliwa Marekani kwa kipindi kirefu kama mshirika wao wa jadi ", Sebastian Arcos ameeleza.

Kwa mujibu wa Sebastian Arcos, wapinzani wengine wanaamini kuwa kufufuliwa kwa uhusiano kati ya Havana na Washington ni jambo zuri kwa sababu serikali ilipo madarakani haitawatuhumu tena kwamba wanatumiwa na Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.