GUATEMALA-RUSHWA-UCHUMI-SIASA-SHERIA

Guatemala: Rais wa zamani Otto Perez amelala usiku wake wa kwanza gerezani

Otto Perez Molina, rais wa zamani wa Guatemala, baada ya kutangaza kujiuzulu kwake na kabla ya kufungwa kwake, Alhamisi hii, Septemba 3 mwaka 2015.
Otto Perez Molina, rais wa zamani wa Guatemala, baada ya kutangaza kujiuzulu kwake na kabla ya kufungwa kwake, Alhamisi hii, Septemba 3 mwaka 2015. REUTERS/Jorge Dan Lopez

Otto Perez Molina amewekwa kizuizini, masaa kadhaa baada ya kujiuzulu kwake, Alhamisi, Septemba 3, katika kambi ya jeshi. Hali hii inatokea wakati zikisalia siku tatu kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Jumapili Septemba 6.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Bunge la nchini Guatemala limemuapisha rais mpya Alehandro Maldonado, aliye kuwa Makamu wa rais wa nchi hiyo.

Maldonado, mwanasheria na mthibitishaji, mwenye umri wa miaka 79, alikua mpaka mwezi Mei mmoja wa wajumbe watano wa Mahakama ya Katiba, kabla ya kuteuliwa kuwa makamu wa rais akichukua nafasi ya Roxana Baldetti aliyejiuzulu kishaaliwekwa rumandekwa muda kwa yuhuma zinazohusiana na faili hiyo ya rushwa zinazomkabili Otto Pérez.

Otto Perez anatuhumiwa na upande wa mashtaka na Tume ya Umoja wa Mataifa dhidi ya kutoadhibu (CICIG) kwa kuongoza mfumo wa rushwa ndani ya Idara ya Forodha ambapo maafisa walikuwa wakipewa hongo kwa kusamehe kodi za baadhi ya vifaa kutoka nje.

Kiongozi huyo wa kihafidhina, aliyekua madarakani tangu mwaka 2012, alisikilizwa Alhamisi wiki hii na jaji Miguel Angel Galvez, ambaye alitoa Jumatano Septemba 2 kibali cha kukamatwa dhidi yake, na kuomba rais huyo kujiuzulu kwa haraka, ili aweze kusikilizwa.

Bunge la nchi hiyo lilimuidhinisha jaji mstaafu wa mahakama kuu, Alehandro Maldonado kuchukua nafasi ya urais, ambapo ameapishwa hapo jana na kuapa kurejesha utawala bora pamoja na kupambana na vitendo vya rushwa.

Saa chache baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi ya urais, Otto Perez alikamatwa na polisi ambapo kwa siku nzima ya jana alikuwa akijibu maswali toka kwa waendesha mashtaka waliotaka kujua kuhusu tuhuma mbalimbali za rushwa zinazomkabili.

Pereza anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kutakaisha fedha pamoja na kutoa misamaa ya kodi kwenye maeneo ya mipaka ya nchi hiyo kwa lengo la kujilimbikizia mali kupitia makampuni yake yanayojihusisha na biashara za mpakani.

Hata hivyo Perez amekanusha tuhuma zote dhidi yake akisema zimechochewa kisiasa na kwamba atahakikisha anapambana kusafisha jina lake.